Steven mushi mushi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2016
- 533
- 739
Hawa ni madj waliojizoelea umaarufu mkubwa ukanda huu wa Africa mashariki kutokana na umahiri wao wa kutafsiri muvi mbalimbali iwe za kihindi, kichina na za kimarekani na nyinginezo ni DJ MARK wa Tanzania na DJ Afro kutoka nchini kenya. Hebu tiririka mdau ni nani mkali wako kati ya hawa madj wawili. Mimi binafsi nawakubali wote kwa kila mmoja na nafasi yake, dj mark ni mkali kwa kutangaza movie za action ee bana ee huyu jamaa utamkubali mwenyewe yaani yuko vizuri kwenye action movie asikwambie mtu na dj Afro yeye namkubali kwa kutafsiri film za mapenzi kama za kihindi na nyinginezo na anavyojua tena kuwa manjonjo kwa kiswahili chake cha kikenya hapo ndo balaa. Kwa upande wako ni nani mkali?