Brooklyn
JF-Expert Member
- Mar 17, 2009
- 1,459
- 286
Leo ilikuwa zamu ya DJ kutoka Tanzania kuwaburudisha washiriki wa shindano la Big Brother Africa. Kwa kawaida Multichoice huwa wanaaalika maDJ kutoka nchi wa
shiriki kila jumamosi saa 5 mpaka saa 6 usiku kuwarusha majoka washiriki wa BBA.
Leo DJ kutoka Tanzania ambaye pia ni radio DJ wa Clouds FM, DJ PQ alipata nafasi ya kuwa burudisha washiriki. Cha ajabu huyu DJ ameonesha umbulula wa hali ya juu kabisa kwa kutopiga nyimbo ya Tanzania hata moja zaidi ya nyimbo ya mshiriki kutoka Tanzania aitwaye Feza kama dedication kwake.
Badala yake 80% kapiga nyimbo za Nigeria hasa za Psquare. Hili limenishangaza sana kwani hakuna nyimbo yoyote ya bongo flava yenye hadhi ya kupigwa ndani ya jumba la BBA?
Mbona ma DJ wengine waliotangulia wiki za nyuma walipiga nyimbo mbili ama tatu za nchini mwao? Hata DJ wa Kenya alipiga za kwao pamoja na Tanzania mfano alipiga nyimbo ya Kesho ya Diamond na ya AY.
Tafsiri yangu ni kuwa huyu mbulula hana confidence kabisa, licha ya mabosi wake Clouds FM kuhubiri umuhimu wa kutumia vizuri fursa "opportunity" lakini huyu DJ somo halijamuingia.
Hii inafanya watizamaji wa nchi zingine wahisi kwamba Tanzania hakuna wanamuziki na kwamba tuwasikiliza Psquare tu.
Ngoja nikope msemo wa Clouds FM kwa kumalizia "MADE IN TANZANIA".