Dk. Bashiru ampa elimu ya uongozi Freeman Mbowe

Dk. Bashiru ampa elimu ya uongozi Freeman Mbowe

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Dr Bashiru ameacha funzo kubwa sana huko machame yaani kuomba msamaha pale upande wa pili unapokwazika na kauli za vijana wa CCM hata kama zilitafsiriwa ndivyo sivyo.
Dr Bashiru amemuombea msamaha Makonda .

Tumeshuhudia matusi mazito kwa Spika na Rais Magufuli karibu kila siku iendayo kwa Mungu kutoka kwa wabunge vijana wa Chadema na wafuasi wao mitandaoni lakini kamwe hutasikia wakikemewa na uongozi wa chama hiko au maaskofu kama Baba Askofu Shoo.

Dr Bashiru amefungua ukurasa mpya wa kukemea aghalabu hata kauli tata za wanaccm Je ni lini katibu au kiongozi wa chadema atasimama mbele ya umma au madhabahu kuwaombea msamaha kina Lissu,Sugu,Mdee,Bulaya na wengine kama kina Mdude?

Tuachane na double standards!!
Mbowe jifunze kuwakemea vijana wako wanaotoa matusi mtandaoni na bungeni ,usisubiri mpaka watekwe.
 
Baba Askofu Shoo...amemaliza kila kitu... Kama hujamuelewa vizuri.. Rudi kwa Katibu Mkuu wa Chama...ni muelewa atakufafanulia kwa upole utaelewa...

Atachoka kuwaombea msamaha msipobadilika.

Jitafakarini...kuomba au kuombewa msamaha kila mara au wakati ni tatizo....sio dalili njema

Bado una nafasi ya kutafakari ujumbe wa Baba Askofu.....tumia muda kidogo kutafakari utamuelewa.[emoji41]
 
Tangu lini?
Mara nyingi, Amekua akithubutu kuongea ambayo wan CCM wengi hawathubutu.

Haonyeshi kutetea upumbavu kwa misingi ya Hofu au Unafiki.

Anaonekana kukemea Uovu pasi kuweka mbele Unazi wa UChama.
 
Mara nyingi, Amekua akithubutu kuongea ambayo wan CCM wengi hawathubutu.

Haonyeshi kutetea upumbavu kwa misingi ya Hofu au Unafiki.

Anaonekana kukemea Uovu pasi kuweka mbele Unazi wa UChama.
Dk Mashinji naye awe hivi
 
Kuwateka Ndio solution??? Alie ombewa msamaha Naona kaonyesha sura yake halisi
 
Dk Mashinji naye awe hivi
CCM SIO CHAMA Cha kujilinganisha na Chadema au vyama vyovyote vya Upinzani.

Kulialia sijui Mashinji aweje ni kupoteza Muda. CCM ambao ndio wanadola, Pesa, Jeshi, media nk ndio wanatakiwa kua na viongozi makini ili kuzipa heshima nyadhifa zao.

Tundu Lisu, Mashinji, Zitto, Mbatia, Mbowe, waongee ama wasiongee wale hawana impact kubwa kwakua hawana dola. Ile itakua to the detriment of their own political parties. Lakini hawa wenye nchi wakiiongea ujinga itakua ni kwa hasara ya taifa.

Kauli za Bashite zilikua za Vijiwe vya Kahawa. Kwa kiongozi mkubwa kama yule, Alipaswa kunolewa ili aongeapo aje na kitu kimeshiba na kina mashiko na sio porojo za mitaani zilizokosa takwimu na kujaa ubaguzi na chuki. Nisiseme sana maana walishamsamehe kwa lile kosa lake. Imeisha.
 
Mbona vijana wa Lumumba usiku kucha mchana kutwa wanamtukana Mbowe hapa JF na wewe Etwege ndiye unaongoza kwa kumtukana na kumkashifu Mh. Mbowe.
 
Lissu ndiye anayetakiwa Kuombwa msamaha.

Hii ni hatari sana. Watu wamekuwa vipofu mpaka wanaona kuwa alichofanyiwa Lissu lilikuwa ni sahihi. Mungu yupo and time will tell. Haiwezekani wakamsababishia kirema mtu halafu yaliyekuwa na afya yake njema halafu wao wakabaki salama mpaka siku ya mwisho. Mungu anajua namna ya kubalance equestions.
 
Mimi naomba orodhesha hayo unayoita matusi kutoka kwa wabunge wa chadema
 
Mfa maji haishi kutapatapa .hio elimu bora atumie mwezi mzima kumfundisha yule dogo aliyevaa jeans iliyochanika kanisani
 
Baba Askofu Shoo...amemaliza kila kitu... Kama hujamuelewa vizuri.. Rudi kwa Katibu Mkuu wa Chama...ni muelewa atakufafanulia kwa upole utaelewa...

Atachoka kuwaombea msamaha msipobadilika.

Jitafakarini...kuomba au kuombewa msamaha kila mara au wakati ni tatizo....sio dalili njema

Bado una nafasi ya kutafakari ujumbe wa Baba Askofu.....tumia muda kidogo kutafakari utamuelewa.[emoji41]
Askofu Shoo anatabia kama Askofu Ngwajima
 
Askofu Shoo anatabia kama Askofu Ngwajima
Askofu Ngwajima tabia yake ni kama ya mkolomije mwenzake Albert Bashite.

Askofu Dk Shoo ni kitu ingine...Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM kakiri mbele yake Jana madhabahuni kuwa ataendelea kuwa mwabafunzi wa Baba Askofu Dk Shoo...


Sasa pata picha hapo.......
 
Acha kufananisha uupuzi wa ufipa na chama kikongwe chenyenye weledi kuhusu makonda hana hekima hata kidogo
Sio ety katafsiriwa vibaya kama anavyo dai nauhakika makonda aliulizwa muda huu kwanini unasema umetafsiriwa vibaya hawezi kujielezea zaidi ya kutoa matusi tu.
Ufipa waki iga busara za viongozi wa ccm ndio wameisha kwani hawana uwezo wa kujenga hoja bila matusi,leo mbowe akitaka amuombee msamaha kiongozi mmoja mmoja itamchukua karne nzima kwani wanachama wake na viongozi wake wanategemea matusi kuwainua kisiasa ndio ujasiri wao mfano mdogo ni mdude.Akimaliza kumtukana raisi anajisifia kuwa ni jasiri.
 
Back
Top Bottom