Dk. Hussein Mwinyi: Nchi za EAC anzisheni Mifuko ya Maendeleo ya Petroli

Dk. Hussein Mwinyi: Nchi za EAC anzisheni Mifuko ya Maendeleo ya Petroli

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mh. Dk. Hussein Mwinyi, amezihamasisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na Mifuko ya Maendeleo ya Petroli, (Petroleum Fund), ambayo itasaidia katika utafiti, ubunifu, mafunzo na uendelezaji wa Sekta ya Mafuta kwa ujumla.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifunga Kongamano na Maonesho ya Petroli Afrika Mashariki (EAPCE’25) ambalo limefanyika kwa Siku Tatu.

Ameeleza kuwa, Dira ya Afrika Mashariki ya 2050 inaelekeza kuhusu kuanzishwa kwa Mfuko huo wa Petroli hivyo huu ni wakati muafaka wa kutekeleza suala hilo kama lilivyoainishwa katika Ibara ya 114 ya Mkataba wa Afrika Mashariki ambayo inaelekeza kuimarisha mashirikiano katika kusimamia rasilimali kwa faida ya wote.
 
Viongozi wa Afrika wanawaza chaguzi kuliko maendeleo.Hivyo kauli au wito wa Rais Mwinyi ni bure kabisa.
 
Back
Top Bottom