"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.
Tumjibu Kigwangala kwa staha badala ya kumshambulia;inawezekana akawa hajui kwa nini tunataka katiba mpya na wala sio hii iliyopo ifanyiwe amendments zaidi!
Kigwangala;
Mimi naona tunataka katiba mpya maana tukisema tuirekebishe hii iliyopo bado tutatia viraka kila sehemu ya na kuifanya iswe tena na uasilia wake!
Mosi;Madaraka ya Rais wa TZ ni makubwa sana;Rais anapaswa kupunguziwa madaraka yake kwa nusu ya asilimia aliyo nayo.Rais asiwe na nguvu ya kuteua TUME YA UCHAGUZI inayosimamia uchaguzi ambao yeye anashiriki;Watendaji wa Rais kama vile Wakurugenzi wa Wilaya wasiwe ndiyo wasimamizi wa chaguzi mikoani na Wilayani!
Pili;Matokeo yanayotangazwa na Tume yasiyo ndiyo ya mwisho kama mgombea aliona kuna nyufa kadhaa zilizosababisha yeye kushindwa;watu wawe huru kwenda mahakamani kupinga ushindi wowote ule kutoka udiwani hadi RAIS
Tatu;Rais aendelee kuteua watendaji wake lkn Bunge ndiyo liwathibitishe na wakivurunda hata kama Rais bado anawahitaji Bunge liwe na uwezo wa kumwambia Rais kuhusu uzembe wa watendaji wake,asipochukua hatua Bunge liwe na uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na watendaji hao!
Nne;Mhimili wa Serikali yaani Bunge liwe na nguvu yake na Rais asiliingilie;Bunge liwe na uwezo wa kukataa hoja za serikali na nguvu yake iendelezwe hadi kwenye idara nyeti za serikali,ni bunge tu ndilo lipewe uwezo wa kuthibiti mapato ya serikali na HAMNA MATUMIZI yatakayaofanywa na serikali bila kupitishwa na Bunge
Tano;Mhakimu na majaji wateuliwe na Rais lkn wathibitishwe na Bunge na wakisha thibitishwa RAIS asiwe tena na uwezo wa kuwaondoa madarakani lkn wanaweza ondolewa na kura ya kutokuwa na imani ndani ya Bunge
Sita;Katiba itamke wazi idadi ya wizara zinazopaswa kuundwa na anayeshinda nafasi ya RAIS;kama katiba labda itasema Mawaziri wawe 20,Makatibu wakuu 20 na hamna manaibu basi lzm sheria hii itekelezwe kama ilivyo
Saba;Misamaha ya kodi ni suala ambalo linapaswa kuingizwa ndani ya katiba;hapo katiba ioanishe ni misamaha ipi inapaswa kutolewa hasa ya kibinadamu tofauti na sasa ambako Waziri tu anaweza jiamulia asemehe kodi
Nane;Ingawaje Rais ndiye amiri jeshi mkuu lkn katiba yetu haisemi lolote uwezo wa Bunge kumdhibiti Rais kuyatumia majeshi yetu vibaya;katiba mpya iseme kuwa ni Bunge tu ndilo litakalopiga kura kulipeleka Taifa vitani,ni bunge tu ndilo litakalo amua jeshi letu likatoe wapi misaada ya kibinadamu;tofauti na sasa ambapo Rais kwa uwezo wake mwenyewe anaweza lipeleka taifa vitani
Nane;Katiba mpya iseme nafasi ya znz huru ndani ya Tanzania;katiba mpya iongelee coalition governamnt iliyoundwa znz;katiba mpya iweke sheria kuhusu jambo hilo kama litakuja kutokea hata bara;na katiba mpya iseme kuwa na serikali tatu tanzania sio dhambi!
Kumi;ni mengineyo mengi sana ambayo kuyataja yote nitajaza kurasa na kurasa,katiba mpya iongelee hata mali asili,michezo,mila,desturi,Utanzania na kumiliki uchumi wao,iongelee hadi hatima ya vizazi vyetu vijavyo!
Kigwangala;
Kwa sababu hizo na zingine nyingi zilizoachwa bado utazidi kusema hujui kwa nini tuandike katiba mpya ?