Shing'weng'we
New Member
- Dec 10, 2010
- 3
- 0
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.
Sishangai kwa post yake.
KWANINI: 1. Ni mbunge wa ccm, tumeona huko nyuma wabunge wa ccm walivyo kejeli honja za msingi kwa nchi yetu!
2. Ni mchanga kwenye siasa
3. Jinsi alivyopata nafasi ya kugombea kupitia ccm inamfanya asiwe kwenye nafasi nzuri ya kutao mchango wenye mawazo kinyume na mtizamo wa chama chake kwa sas
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.
.....but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?.
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.
The issues: 1. Madaraka ya rais ni makubwa mno hususani katika uteuzi wa viongozi wa nafasi nyeti. 2. Wateule wote wa rais wanapaswa waidhinishwe na bunge ili wawajibike kwa bunge. Wateule kama jaji mkuu na wakuu wa majeshi 3. Nafasi za makamu wa rais,manaibu waziri,wakuu wa mikoa na wilaya ni redundant na wasteful of state resources,ivyo zifutwe. 4. Rais aapishwe miezi 3 baada ya matokeo kutangazwa ili kutoa fursa ya kupinga matokeo mahakamani. 5. Tume ya uchaguzi iwe huru na viongozi wake wawajibike kwa bunge,na iwe na wafanyakazi wa kudumu waajiriwa,wakiwamo wasimamizi wa uchaguzi majimboni,na sio wakurugenzi kama ilivyo sasa. 6. Itikadi ya dola iwekwe wazi,aidha ujamaa au ubepari. 7. Rais hasiwe na mamlaka na uamuzi wa mwisho juu ya ardhi na matumizi yake. Hiyo iwe kazi ya bunge kwani ndio sauti ya wananchi. 8.Suala la wabunge kupita bila kupingwa lisitishwe,na pawepo na kura za ndio na hapana inapojitokeza hali ya kuwepo mgombea 1. 9. Nafasi 10 za uteuzi wa rais wa wabunge zifutwe,hazifuati misingi ya demokrasia. 10. Nafasi za makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa halmashauri,miji,wilaya na majiji ziwe za kugombaniwa yaani za kuaajiriwa. 11. Mawaziri wateuzi wasiwe wabunge,na uteuzi wao lazima uidhinishwe na bunge. 12. Maamuzi makubwa ya rais,kama ya kuanzisha au kufuta nafasi za madaraka mbalimbali katika utumishi wa umma, lazima yaidhinishwe na bunge. 13. Katika uchaguzi mkuu na mdogo,mshindi wa urais,ubunge udiwani,uenyekiti wa kijiji au mtaa,lazima awe amepata asilimia 50 ya kura kutokana na idadi ya waliopiga kura. 14. Iwepo nafasi ya wagombea huru kushiriki katika chaguzi kuu na ndogondogo,katiba iwekwe wazi. 15. Kuwe na wizara za kudumu ambazo hakuna rais atakaeweza kuzibadili,ziwe za fedha, elimu,ulinzi,afya,kilimona mazingira,maliasili na utalii,nishati,maendeleo ya jinsia na ustawi wa jamii,michezo na utamaduni,mambo ya ndani,mambo ya nje na wizara ya sayansi na teknolojia. Hizi ndo issues zinazonifanya nitake na kudai KATIBA MPYA.
Rekebisho la kwanzaQUOTE=MkamaP;hizo zote ni sababu moja tu, ambayo inahitaji marekebisho mawili tu ktk katiba iliyopo.
Marekebesho mawili yepi? Pia toa sababu zako nawewe. Don't be a critic with no ANSWERS,unless you are a POLLUTER by making NOISE.
"Many people are claiming and advocating for a new constitution, but most don't give reasons why? Why do you think we need a new constitution? or Major changes in the current constitution? What are the issues people?" Kutoka post yake kwenye facebook.
Tumjibu Kigwangala kwa staha badala ya kumshambulia;inawezekana akawa hajui kwa nini tunataka katiba mpya na wala sio hii iliyopo ifanyiwe amendments zaidi!
Kigwangala;
Mimi naona tunataka katiba mpya maana tukisema tuirekebishe hii iliyopo bado tutatia viraka kila sehemu ya na kuifanya iswe tena na uasilia wake!
Mosi;Madaraka ya Rais wa TZ ni makubwa sana;Rais anapaswa kupunguziwa madaraka yake kwa nusu ya asilimia aliyo nayo.Rais asiwe na nguvu ya kuteua TUME YA UCHAGUZI inayosimamia uchaguzi ambao yeye anashiriki;Watendaji wa Rais kama vile Wakurugenzi wa Wilaya wasiwe ndiyo wasimamizi wa chaguzi mikoani na Wilayani!
Pili;Matokeo yanayotangazwa na Tume yasiyo ndiyo ya mwisho kama mgombea aliona kuna nyufa kadhaa zilizosababisha yeye kushindwa;watu wawe huru kwenda mahakamani kupinga ushindi wowote ule kutoka udiwani hadi RAIS
Tatu;Rais aendelee kuteua watendaji wake lkn Bunge ndiyo liwathibitishe na wakivurunda hata kama Rais bado anawahitaji Bunge liwe na uwezo wa kumwambia Rais kuhusu uzembe wa watendaji wake,asipochukua hatua Bunge liwe na uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na watendaji hao!
Nne;Mhimili wa Serikali yaani Bunge liwe na nguvu yake na Rais asiliingilie;Bunge liwe na uwezo wa kukataa hoja za serikali na nguvu yake iendelezwe hadi kwenye idara nyeti za serikali,ni bunge tu ndilo lipewe uwezo wa kuthibiti mapato ya serikali na HAMNA MATUMIZI yatakayaofanywa na serikali bila kupitishwa na Bunge
Tano;Mhakimu na majaji wateuliwe na Rais lkn wathibitishwe na Bunge na wakisha thibitishwa RAIS asiwe tena na uwezo wa kuwaondoa madarakani lkn wanaweza ondolewa na kura ya kutokuwa na imani ndani ya Bunge
Sita;Katiba itamke wazi idadi ya wizara zinazopaswa kuundwa na anayeshinda nafasi ya RAIS;kama katiba labda itasema Mawaziri wawe 20,Makatibu wakuu 20 na hamna manaibu basi lzm sheria hii itekelezwe kama ilivyo
Saba;Misamaha ya kodi ni suala ambalo linapaswa kuingizwa ndani ya katiba;hapo katiba ioanishe ni misamaha ipi inapaswa kutolewa hasa ya kibinadamu tofauti na sasa ambako Waziri tu anaweza jiamulia asemehe kodi
Nane;Ingawaje Rais ndiye amiri jeshi mkuu lkn katiba yetu haisemi lolote uwezo wa Bunge kumdhibiti Rais kuyatumia majeshi yetu vibaya;katiba mpya iseme kuwa ni Bunge tu ndilo litakalopiga kura kulipeleka Taifa vitani,ni bunge tu ndilo litakalo amua jeshi letu likatoe wapi misaada ya kibinadamu;tofauti na sasa ambapo Rais kwa uwezo wake mwenyewe anaweza lipeleka taifa vitani
Nane;Katiba mpya iseme nafasi ya znz huru ndani ya Tanzania;katiba mpya iongelee coalition governamnt iliyoundwa znz;katiba mpya iweke sheria kuhusu jambo hilo kama litakuja kutokea hata bara;na katiba mpya iseme kuwa na serikali tatu tanzania sio dhambi!
Kumi;ni mengineyo mengi sana ambayo kuyataja yote nitajaza kurasa na kurasa,katiba mpya iongelee hata mali asili,michezo,mila,desturi,Utanzania na kumiliki uchumi wao,iongelee hadi hatima ya vizazi vyetu vijavyo!
Kigwangala;
Kwa sababu hizo na zingine nyingi zilizoachwa bado utazidi kusema hujui kwa nini tuandike katiba mpya ?