Dk Kimei (CRDB) kuwania tuzo ya kinara benki Afrika

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei amechaguliwa kwenye mchakato wa kumtafuta Kinara wa Benki Afrika kwa mwaka 2013.

Mchakato huo unaendeshwa na African Banker Awards chini ya African Development Bank Group.

Kinara wa benki wa mwaka, ni tuzo inayotolewa kwa viongozi (CEO`s) wa sekta ya benki na fedha barani Afrika, ambao wamepata mafanikio makubwa kwenye mashirika yao hivyo kuleta maendeleo kwenye sekta fedha na uchumi kwa nchi zao.

African Banker Awards imechagua vinara watano wa sekta ya fedha Afrika kuingia katika mchakato huo, mmoja wao ndiye atakayejitwalia tuzo hiyo.

Zaidi ya Dk Kimei, wengine waliongia kwenye mchakato huo na nchi wanazotoka kwenye mabano ni Segun Agbaje wa GTB Bank (Nigeria), Aigboje Aig wa Imoukhede-Access Bank (Nigeria), Andrew Allly wa Africa Finance Corporation (Nigeria) na Jao Figuerdo wa Unico Bank.

Dk Kimei ni Mtanzania wa kwanza kuingizwa kwenye mchakato huu tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo zaidi ya miaka kumi iliyopita, npia ni pekee kwenye kinyang'anyiro hicho ambacho kimekuwa kikitawaliwa na benki kutoka Nigeria na Afrika ya Kusini.

Dk Kimei ambaye ni mchumi mwenye Stashahada ya Uzamivu, amefanya kazi sekta ya fedha kwa zaidi ya miaka 30 akitokea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alikokuwa Mkurugenzi wa Sera na Utafiti kabla ya kujiunga CRDB mwaka 1998 kama Mkurugenzi Mkuu.

Akiwa CRDB ameiongoza kutoka benki iliyokuwa ikijiendesha kwa hasara hadi inayoongoza nchini.

Benki hiyo imefanya marekebisho mbalimbali, ambayo yameiletea mafanikio na kuwa miongoni mwa benki zinazoongoza nchini.


Chanzo: Mwananchi


My Take;
CRDB chini ya Dr Kimei ni benki ambayo imetumika kisiasa yaani imekuwa ikishirikiana na mafisadi ndani ya utawala wa CCM. Katika tukio la EPA benki hiyo inayoelezwa kuwa ni ya wazawa ilihifadhi fedha zailizochotwa (zilioibiwa) kutoka BoT na wale wezi naye akakaa kimya.

Katika ule mchoto wa Kagoda mabilioni yaliwekwa katika akaunti sita za matawi ya benki hiyo na baadaye kuchotwa na watu eti hadi leo hawajulikani hadi leo!!! Hii inawezekana kwa benki kubwa kama hiyo kutojua ilimlipa nani mabilioni hayo na zile akaunti alizifungua nani?

Pili CRDB chini ya Kimei iliisaidia sana kampuni feki ya Richmond kuwapatia guarantee ya letter of credit kuisadidia ufisadi wao.

Kwa hali hii Dr Kimei hafai kupata tuzo hiyo.

Nawasilisha.
 
Mchango wa Benki katika ukuaji wa Uchumi ni Muhimu. Ni lazima vigezo vya Tuzo vihusishe mchango wa benki katika kukabiliana na ufisadi.

Benki inayowezesha ufisadi,usafirishaji wa fedha haramu n.k ni benki ambayo imekosa umaarufu wa maadili ya kibenki.Ubora wa Benki hiyo na management nzima unapungua
 
Kila la kheir Dkt Kimei Unastahili hiyo heshima, kosa moja au mawili hayamfanyi kutokuwa Bora. Kimei anastahili hata kuwa GAVANA jamaa anajielewa na anaeleweka!
 
katika hili ninakubaliana na wewe, Benki hii imejaa rushwa katika uendelezaji wa shughuli zake.

Mfano hai ni mimi mwnyewe katika biashara zangu nilitaka udhamini katika mradi wangu kwa kiasi cha shs milioni mia tatu na nikaweka dhamani nyumba zangu.

Pamoja na kuzungushwa sana na kutengeneza valuation reports, idara ya mikopo na dhamana walikataa. KISA, sikutoa kitu kidogo kwa vijana wa idara hiyo.

Ningependa Kimei alijue hilo, kuwa yeye ni kinara aliyekaa juu ya uozo wa ufisadi benkini kwake.
 
Hawa ndiyo wale viongozi waliosoma sana nchini lakini elimu zao hazitumiki "Professionally"kusaidia wananchi. Zaidi zinatumika kisiasa kulaghai wananchi wengi na kufurahisha au kutumikia wachache ndani ya chama tawala.

Ukitaka kupima udhaifu wa uongozi wa mashirika haya jaribu kupata huduma kutoka kwao bila kuwa na kijibarua cha utambulisho kutoka kada wa CCM au mtu anayefahamika kwao. Utazungushwa na kuishia kupata hasara zaidi.

Mambo kama haya ni vyema yakawa yanapelekwa huko kwenye hivyo vyombo husika na ushahidi wa kutosha ili wasiendelee kuzihadaa jumuiya za kimataifa.
 
Haya mataifa yaliyoendelea ni wezi wakubwa, wanacreate migogoro maeneo mbalimbali duniani ili kupata mianya ya kuiba rasilimali, pesa hizo tunaenda kuwaomba au kuwakopa huku tukijua hizo ni pesa za damu ya wa-Iraq, wa-Congo, wa-Laiberia n.k.

Matajiri wengi (sio wote) wamejaa dhuluma, ufisadi, fitna wafike walipo na walinde utajiri wao. Kwa hiyo kama hii tunzo inatolewa kwa kuangalia how fare you are in your bussnes then you are right.
 
Kama kuna benki mbovu na ya hovyo zaidi nchini basi ni CRDB. Nilianza kuidharau kipindi kile cha EPA ambapo mwanzoni Kenya Commercial Bank (KCB) waliona mtiririko usio wa kawaida wa ufunguaji akaunti na uwekaji hela wakakataa na kuitaarifu BoT.

Mafisadi yalivyoona hivyo wakaamua kupitishia pesa haramu CRDB (eti benki ya wazawa!) wakifungua akaunti hadi siku za mapumziko; labda baada ya kuona hivyo na ili waweze kuendelea na ufisadi wao ndio maana wameamua baadhi ya matawi ya-operate hadi sikukuu ili wapate utetezi mbele ya sheria huko tuendako; kuna siri zaidi ya tunavyodhani ni kumjali mteja.

Kama mchango wangu kwa taifa, nilichoweza kufanya ni kufunga mara moja akaunti yangu niliyokuwa nayo CRDB mara baada ya ile kashfa ya EPA japo haikuwa na hela ya maana. Lakini angalau nilionesha hisia zangu hata kama ni kilio cha samaki.

Hata hivyo, nikiri kwamba, pamoja na kufunga akaunti yangu, lakini kwa namna moja ama nyingine "inanilazimu" kutumia huduma za CRDB hasa kama kulipa ada za watoto, n.k. Huduma zao bado ni bomu mno. Inaweza kukuchukua hata saa nzima kumfikia teller hata kama kwenye queue ni mtu wa tatu. Jibu rahisi ni MTANDAO UNASUMBUA.

Eti benki ya aina hii, BENKI ISIYO NA JINA, ndio inawania nafasi ya benki bora Africa! Pathetic! Anayefahamu kirefu cha CRDB atufahamishe.
 
maana ya jina la benki hii na shughuli inazofanya haziendani,benki ya maendeleo vijijini leo hii iko mjini tu ikitumikia mafisadi,matajiri na wala si wakulima na makabwela.
 
CRDB Inaongoza nchini kwenye nini?
mimi najua NMB NDI Bank kubwa kwa kila kitu
 
Kila la kheir Dkt Kimei Unastahili hiyo heshima, kosa moja au mawili hayamfanyi kutokuwa Bora. Kimei anastahili hata kuwa GAVANA jamaa anajielewa na anaeleweka!

Nina mengi ya kusema lakini naanzia na hilo la ugavana: HAFAI HATA KIDOGO
 
Kila la kheir Dkt Kimei Unastahili hiyo heshima, kosa moja au mawili hayamfanyi kutokuwa Bora. Kimei anastahili hata kuwa GAVANA jamaa anajielewa na anaeleweka!

We utakuwa fisadi
 
maana ya jina la benki hii na shughuli inazofanya haziendani,benki ya maendeleo vijijini leo hii iko mjini tu ikitumikia mafisadi,matajiri na wala si wakulima na makabwela.

Mkuu poe sana unaonekana hufuatilii mambo. Hakuna Benki ya Maendeleo Vijijini wala CRDB siyo benki ya ushirika na maendeleo vijijini hii ni CRDB Plc.

Zamani hii benki ilikuwa ikiitwa Cooperative and Rural Development Bank wakati huo ikimilikiwa na serikali ila baadaye ikabinafsishwa na kubadili jina na kuitwa CRDB Bank Ltd (CRDB kama jina linalojitegemea na wala si kifupi cha jina lile la benki ya ushirika na maendeleo vijijini) na baadaye ikaitwa CRDB Plc.

Mkuu unarudi kwenye Ujamaa; kuna ushirika gani siku hizi?
 
Nirekebishe kidogo.

Sina ushirika na Kimei, natoa mchango kama mtanzania na kama mdau katika sekta ya fedha.
  • Dr. Kimei ndiye mkurugenzi mtanzania pekee kuendesha benki kubwa nchini kwa mafanikio.
  • CRBD imepata mafanikio makubwa kutoka benki mufilisi na sasa ni benki inayoongoza kwa amana na benki ya pili kwa faida baada ya NMB. Kwa mwendo wa CRDB, siku si nyingi itashika namba moja kwa upande wa amana na faida.
  • Wamiliki wa CRDB, ambao wengi kwa idadi ya hisa ni wageni, wameridhika na utendaji wa Dr. Kimei. Linganisha mafanikio ya CRDB na benki kubwa zinazoongozwa na wageni kama NMB, NBC, Standard Chartered, Barclays, Citi kisha njoo uonyeshe ubaya wa Kimei.
Mwisho, naendelea kuona jinsi gani mchawi wa Mtanzania ni Mtanzania mwenyewe. Watu wanampinga Kimei, mtu wao, bila hata kujua hao wageni ni watu gani! Kwao ni bora apate mgeni wasiyemfahamu kuliko kufaidi huyu Kimei. Kumbukueni akipata Kimei, Tanzania inapata fursa nyingine ya kusomeka kwenye vyombo vya kimataifa, ndivyo mambo yanavyokwenda.
 

Mkuu CRDB ndio jina lenyewe na wala halina kirefu! Inaitwa CRDB Plc.

Kimei na vijana wake Directors/Managers wapo Arusha wanakula faida
 
maana ya jina la benki hii na shughuli inazofanya haziendani,benki ya maendeleo vijijini leo hii iko mjini tu ikitumikia mafisadi,matajiri na wala si wakulima na makabwela.

Hilo jina lenyewe linaonesha benki yenyewe isivyokuwa na vision ya maana. Wanajidai kuiita "CRDB Bank" (Co-operative and Rural Development Bank Bank); wizi mtupu - hamna kitu hapo. Kimsingi jina CRDB lilibeba maana iliyokusudiwa enzi za Mwalimu tofauti na manyang'au wa leo wanavyolichukulia - limebaki jina tu kama hadaa kwa wananchi lakini malengo ni tofauti kabisa.
 
kwa nini hafai kuwania tuzo ilo kwa sababu mchaga? kama sakata la EPA wahusika wanajulikana SERIKALI YA CCM (MKAPA NA KIKWETE) Kimei ni mkurugenzi awezi akabagua wateja wake au kuwafanyia uchunguzi kujua wezi hii ni sawa na wakili kamanda MARANDO alipowatetea mafisadi wa epa mahakamani. DR KIMEI GO GO.
WISH YOU ALL THE BEST.
 

Money Laundering

Sent from my BlackBerry Z10 using JamiiForums
 
Binafsi naikubali sana CRDB bank huduma zao ni bora kuliko benk zote nilizowahi kuzitumia NMB na NBC.hayo mengine ya ufisadi nawaachia wenyewe.
 
Mkuu CRDB ndio jina lenyewe na wala halina kirefu! Inaitwa CRDB Plc.

Kimei na vijana wake Directors/Managers wapo Arusha wanakula faida

Duh! Hii kali. Kwa hiyo CRDB ni neno la kiwapi hilo Mkuu? Ni kichina, kisukuma, kireno, au? Kama ni la Kiswahili, kwa mara ya kwanza Kiswahili kimepata neno linaloundwa na "makonsonanti" matupu; kama ni Kiingereza basi kimepata neno la kwanza linaloundwa na consonants tupu zaidi ya tatu! Huu ni ubabaishaji ulikubuhu kwa viwango vyote. Linapaswa kuingizwa kwenye kamusi ya lugha husika kama neno jipya!

Kumbe ndio maana wanaiita CDRB Bank? I thought ile "B" ilimaanisha "Bank" kumbe ni sehemu ya neno lenyewe na ndio maana inafahamika kama CRDB Bank; ha ha ha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…