mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,126
- 5,068
Juzi, Rais Samia alifanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri kwa kutengua uteuzi wa mawaziri watatu akiwamo Ndugulile na kuteua wapya wanne ambao ni Dk Ashatu Kijaji, Dk Stergomena Tax, January Makamba na Profesa Makame Mbarawa.
Ndugulile uteuzi wake ulienguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Dk Kijaji ambaye ni mbunge wa Kondoa Vijijini.
Ndugulile, jana Jumatatu Septemba 13, 2021, kupitia mtandao wa kijamii aliandika;
“Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. Nawashukuru Wizara na taasisi zake kwa ushirikiano walionipa. Nashukuru wadau wa Tehama kwa ushirikiano mlionipa. Hongera sana Dk Ashatu kwa kuteuliwa. Kazi Iendelee”