Dk. Salim: Suala la uraia wa nchi mbili litatuliwe

Dk. Salim: Suala la uraia wa nchi mbili litatuliwe

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
[h=2][/h]





Salim%20A%20salim.jpeg


Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Salim Ahmed Salim



Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Salim Ahmed Salim, amelitaka Baraza la Katiba Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuyapa uzito maoni ya Watanzania walioko nje ya nchi kuhusu suala la uraia wa nchi mbili na kuangalia jinsi ya kuyapatia ufumbuzi.

Dk. Salim Ambaye pia ni Waziri Mkuu msataafu na Katibu Mkuu mstaafu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Baraza hilo, ambao ulihudhuriwa na Mabalozi wastaafu, wafanyakazi wa wizara hiyo pamoja na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo.

Alisema kabla ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume hiyo na hata baada ya kuteuliwa, amekuwa akisafiri mara kwa mara na kukutana na Watanzania ambao wanaishi nje ya nchi na wengi wao wamekuwa wakizungumzia kuhusiana na suala la uraia, na wanalizungumzia zaidi suala la uraia wa nchi mbili, hivyo wizara hiyo inaweza kusaidia sana kwa kutoa mchango wake kutokana na uzoefu uliopo.

Aidha Dk Salim aliongeza kuwa wizara hiyo ina nafasi nzuri zaidi ya kuchambua na kushauri jinsi ya kutumia vizuri rasilimali za nchi kuendana na uzoefu walioupata kutokana na kufuatilia na kutembelea nchi nyingine duniani.

Akizungumzia suala la Muungano, alisema wizara hiyo ipo katika nafasi nzuri ya kuchangia katika suala la katiba gani inahitajika kwani moja ya dukuduku kubwa la Wazanzibari ni kwamba Muungano kwa ulivyo sasa hauwapi nafasi ya kutambulika, na kupata ushirikiano katika medani ya kimataifa hasa kwa yale mambo ambayo si ya Muungano.

“Muundo wa Muungano umekuwa ni jambo ambalo limejadiliwa sana na kuonyesha tofauti kubwa kwa wachangiaji mbalimbali, kutokana na uzoefu wenu wa mambo ya nchi za nje na mchango wenu kama wizara inayotetea maslahi ya Tanzania kwa ujumla, na uzoefu uliopatikana mpaka sasa mnaweza mkachangia vizuri pia katika suala la Muungano,” alisema.




CHANZO: NIPASHE
 
Hatutaki uraia wa nchi mbili maana wahindi ndo wameshupalia vibaya, toka lini kutumikia mabwana wawili kama si unafki? kama upo huko kaa huko na kama upo huku kuwa wa huku, Salim kwa hilo tuheshimiane kabisa na msifikiri hatujui kuwa waziri wa mambo ya nje ana uraia wa Canada
 
Ni vema kunyamaza kuliko kutolea maoni jambo usilolifahamu vizuri.

Mkuu ingekuwa ni vizuri kama ungetufahamisha. Lakini ukiangalia kwa undani sasa hivi kuna baadhi ya watu huwa wanakuja kutoka kwenye nchi zao na kuomba uraia wa Tanzania, wakijua kuwa wanaweza kuupata kwa urahisi. Wakiwa hapa Tanzania wanatutukana, wanatukejeli na hata kutuibia na kutudhalilisha, halafu baada ya miaka tisa wanenda kuishi Ulaya, Canada na marekani kwa kutumia passport yetu.

Watu hao wanatutumia tu. Na wanataka wawe na uraia wa nchi mbili ili waweze kuwa raia wa nchi zao na huku wakiwa na passport ya Tanzania.

Kwa watanzania wazawa wazalendo, hao ni case nyingine. Kuna wengine wanaenda kutafuta maisha nje wakitokea hapahapa Tanzania. Lakini baada ya kujilipua ili wapate convinience huko, wanakuwa na matatizo. watu kama hao ndio wanatakiwa kufikiriwa kwenye mabadiliko ya katiba, sio wale wanaotuibia.
 
Hakuna mtu yeyote aliyekatazwa kuwekeza Tanzania ati kwa sababu tu si raia wa Tanzania. Tunao wawekezaji kwenye miradi midogo na mikubwa kama ya migodi, mahoteli nk ambao si raia wa Tanzania; wanachotakiwa kufanya ni kufuata taratibu na sheria zetu.

Pia hao watanzania walioko nje, wako huko kwa kuwa kuna shughuli wanazofanya huko ambazo zinakubalika kwa sheria na taratibu za huko; iwe ni kuwekeza, kuajiriwa nk.
Kwa mantiki hayo kuwa raia au kutokuwa raia hakumzuii mtu yeyote kufanya shughuli yoyote halali kwa kufuata taratibu na sheria za nchi husika.
Watanzania walioko nje wanaweza kuwa wanataka uraia wa nchi mbili kwa kuwa taratibu za huko waliko au za huku ziliwalazimisha waukane uraia wa Tanzania ili waweze kuwekeza huko. Hizo ni sheria na taratibu za sehemu husika ambazo wamezifuata na kufanikiwa -very good. Wakitaka kurudi kuja kuwekeza Tanzania, hatuwakatazi wala hatuwalazimishi kuwa tena raia wa Tz wala hatuwachukii eti kwa sababu waliukana uraia wa TZ. Tunawapokea kama tunavyowapokea wachina, wasouth, wamarekani nk. Na huku watafanikiwa kama vile wasio waTZ walivyofanikiwa hapa kwetu au wao walivyofanikiwa huko waliko.
Inawezekana kuna fursa fulani fulani zinatolewa kwa walio raia tu. Katika nchi zote fursa kama hizo huwa ni kwa makundi maalum na kwa sababu maalum; yaweza kuwa ni makundi ambayo yaliumizwa na mifumo iliyokuwepo na sasa ni kujaribu kurekebisha makosa hayo; kwa mfano ubaguzi wa rangi kule afrika ya kusini. Kwa hapa kwetu, wengi tulidumazwa na mfumo wa ujamaa ambao haukushawishi uwekezaji binafsi bali uwekezaji wa kiserikali; hivyo kutoa fursa kwa raia tu ni jitihada za kufufua moyo wa kuwekeza kibinafsi.
Tukichukua fursa hizi kwa makundi hayo, tukaruhusu hata wale walioweza kuwekeza huko nje nao wazitumie (kana kwamba nao bado ni dhaifu) tutajikuta hatumsaidii huyo tunayekusudia kumsaidia; yule mkazi wa buguruni, mabatini, nk. maana atakuja Mmarekani au mchina au mSA nk tutampatia uraia na kwa kuwa atakuwa ni raia basi ana ruhusa ya kutumia fursa hizo. Hakika haitatusaidia. Baba wa Taifa alitoa mifano mingi wakati wa jitihada za kubinafsisha mashirika yetu lakini Mkapa akafunga masikio; kilichotokea tunakijua na tunakiona; tukiruhusu tena ushindanishwaji wa raia wetu walio dhaifu na hao raia kutoka nje (uraia wapili); hawa raia wetu hawatoki huko shimoni.
Tukumbuke pia wizi na ufisadi unaaoendelea katika nchi yetu. Ona namna ambavyo pesa zimefichwa nje na hatuwezi kuzipata; na hao ni raia wa Tz tu, je leo wakipata nafasi ya kuwa raia wa nchi zingine pia, si ndiyo kabisa!!!!
Uki-google mulitiple citzenship utaona kwenye wikipedia kuwa kuna nchi zenye sheria kama za TZ kwamba ukipata uraia wa nchi nyingine basi automatically unapoteza urai wa TZ; baadhi ni nchi nzito kama China, Japan, Denmark, India,Netherlands, Norway nk. Na kama uk haiwezi kuwa na sheria kama za TZ kwa historia yao - UK (united Kingdom); bila kuwa na mataifa mengi uk haipo, itabaki england tu.
Nihitimishe kwa kuwaasa watz wenzetu waliofanikiwa huko nje, kama ni kodi kubwa wanazolazimika kulipa wakitaka kuwekeza tz, wajione kuwa ni kuwawezesha wenzao waliobakia huku; watusaidie kutafakari uchumi wetu utakavyoumizwa tukiruhusu uraia wa nchi mbili. Nimesoma mahali fulani kuwa tunao viongozi ambao wana uraia wa nchi nyingine bila ya kuukana uraia wa TZ; hakika hao wakipata mwanya 'watatunyonga' kabisa; ni kuogopwa kuliko ukoma. Tuwachunguze, kama ndiyo hao wanaopigania uraia wa nchi mbili, tuwanyang'anye uraia wetu na waache uongozi na washtakiwe kwa kuvunja sheria.Kumbukeni masuala kama haya mlituburuza wakati wa kuunda jumuia ya afrika mashariki, mkaingiza nchi nyingine bila ridhaa ya wananchi – matokeo mnayaona; Tembo amejaa kibandani na mwenye kibanda kafukuzwa!

 
What percentage of the total population are Tanzanians living abroad who are yearning for the dual citizenship?
 
What percentage of the total population are Tanzanians living abroad who are yearning for the dual citizenship?

It may be less than 1. But still they are Tanzanians and if that will help them retain their Tanzanianship, why not! Pamoja na kuwa watu wanakuwa nje kutokana na maslahi ya kiuchumi, wengi wana mapenzi na nchi yao.
 
It may be less than 1. But still they are Tanzanians and if that will help them retain their Tanzanianship, why not! Pamoja na kuwa watu wanakuwa nje kutokana na maslahi ya kiuchumi, wengi wana mapenzi na nchi yao.

Kama wana mapenzi na nchi yao, why do they agree to renounce their citizenship in order to acquire foreign citizenship? You cannot eat your cake and still have it!! They just want to double dip basi.
 
Zaidi ya asilimia 50 ya wakazi wa Dubai sio raia wa Dubai ni wakazi tu. lazima tuheshimu uraia wetu tuna miaka 50 tu ya uhuru tunataka tuwe kama marekani!
 
Back
Top Bottom