kasyabone tall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2009
- 254
- 63
Dk. Slaa aivuruga Kamati Kuu CCM
CHADEMA yashtukia mkakati wa kuiba kura zao
na Mwandishi wetu
ZIKIWA zimesalia siku 18 kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu, Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC), imekiri kuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ni tishio, hivyo imepanga mikakati mizito kumkabili, Tanzania Daima Jumatano imebaini.
Moja ya mikakati hiyo ni pamoja na kuwaangukia viongozi na marais wastaafu, mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, ambao sasa wamekubali kwenda kumpigia kampeni Rais Kikwete.
Uamuzi huo wa Kamati Kuu ya CCM, umefikiwa mwishoni mwa wiki wakati wa kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam, ambacho pamoja na mambo mengine, kilifanya tathmini ya mwenendo wa kampeni na kuweka mikakati ya kumkabili Dk. Slaa katika kipindi hiki kilichobaki.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, CC ililazimika kuwaangukia wastaafu hao ambao wamekubali kumpigia debe Kikwete siku chache kabla ya uchaguzi.
Chini ya mkakati huo, CC imeazimia kuongeza nguvu ya fedha na hata kukodisha helikopta nyingine zinakazotumiwa na wastaafu hao na kuongeza matangazo kwenye vituo vya televisheni na redio ili kuwashawishi wananchi wampigie kura Kikwete.
Kwa kifupi CC imekiri kwamba Dk. Slaa ana nguvu na anaungwa mkono na wengi, hivyo wazee; Mkapa, Mwinyi, Malecela na wengine, wanaanza kumpigia kampeni JK na watapita maeneo yale ambayo Dk. Slaa amepita, kilisema chanzo chetu cha habari.
Awali mgombea wa CCM ambaye anatetea kiti chake alikuwa akipita huku na kule akijinadi mwenyewe kama mtoto mkiwa.
Jambo la kustaajabisha ni kwamba wazee na viongozi wengine wastaafu wa serikali zilizopita ambao wanavikwa heshima kubwa na Watanzania, ukiachia siku ya uzinduzi, hawakushiriki kampeni za Kikwete, hali iliyoibua hisia kwamba ama wamewekwa kando kwa makusudi au wamejiweka pembeni wenyewe.
Mbali na Mwinyi na Mkapa kutokuwapo kwenye kampeni, makamu wenye viti wa CCM, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Pius Msekwa Bara, nao wamekacha kampeni hizo.
Mawaziri wakuu wastaafu, Joseph Warioba, Cleopa Msuya, Frederick Sumaye, Salim Ahamed Salim na wengi wengineo, hawajaonekana hata mara moja kwenye majukwaa ya CCM.
Kada pekee aliyebakia Dar es Salaam, Abdulrahman Kinana, akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Mkakati wa Kampeni ya CCM, amekuwa akijibu hoja kwa waandishi wa habari kila inapotokea Dk. Slaa amerusha kombora.
Habari zaidi zilisema kuwa CC pamoja na mambo mengine, ilitumia muda mwingi kujadili kasi ya Dk. Slaa tangu alipoanza kampeni na uwezo alionao kifedha na kujiridhisha kwamba si wa kumbeza kutokana na mvuto wa kisiasa alionao kila alipokwenda.
Hadi sasa CCM imekwisha kutumia mbinu tatu za kutaka kummaliza kisiasa Dk. Slaa na kupunguza kura zake kwa kuibua kashfa na uzushi ili kumchonganisha kwa wananchi bila mafanikio.
Mbinu ya kwanza iliyotumiwa na makachero wa chama hicho tawala ni pamoja na kuibua hoja ya udini kwamba Dk. Slaa anaungwa mkono na Wakristo.
Pia waliibua kashfa ya maisha yake binafsi kuhusiana na mwanamke aliyenaye sasa na anayetarajia kufunga naye ndoa, Josephine Mshumbusi, kwamba ni mke wa mtu. Kesi hiyo sasa ipo katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Pia ameibuliwa hoja kwamba anachochea wananchi kumwaga damu. Katika hoja hiyo, makachero wa CCM wanasambaza ujumbe mfupi kupitia kampuni za simu za mikononi wakidai Dk. Slaa ni mropokaji, anayetaka kumwaga damu.
Hata hivyo Dk. Slaa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wamekana kutoa kauli hiyo na kulitaka Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua viongozi wanaodaiwa kutoa kauli hiyo.
Katika hatua nyingine, CHADEMA imedai kubaini mkakati wa kuiba kura kwa kutumia mtandao wa kompyuta.
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, aliiambia Tanzania Daima Jumatano kuwa tayari wameijulisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), juu ya kuwapo mpango huo na kwamba chama chake kimejiandaa kukabiliana na hujuma hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tayari chama hicho ambacho kinapewa nafasi kubwa ya ushindi kimebaini kuwapo kwa vituo hewa vya kupigia kura na makachero wao wanaendelea na uchunguzi wa kina.
Hata hivyo Mnyika hakutaka kuuweka wazi mkakati huo kwa hofu ya kuwapa wapinzani wao mbinu nyingine ya kuiba kura.
Wakati huohuo, Dk. Slaa amewataka wanachama wa CHADEMA kuwa wa mwisho kuanzisha vurugu kabla na baada ya uchaguzi.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wake wa kampeni, uliofanyika Kibondo, mkoani Kigoma.
Alisema kuwa CHADEMA haitakubali kuona wafuasi wake wakianzisha vurugu na kusisitiza kuwa hata wakichokozwa wasilipe kisasi, kwani CCM itapata kisingizio.
Pia amemtaka Rais Kikwete kuacha kuhubiri amani majukwaani kama hatakuwa tayari kutekeleza azima hiyo kwa vitendo, kwa kuvifuta vikundi vya Green Guard, ambao alisema wamekuwa chanzo cha kuvuruga amani.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ametangaza majimbo ambayo CHADEMA ina uhakika wa kushinda.
Aliyataja majimbo hayo kuwa ni Kigoma Kaskazini, Mhambwe, Kigoma Mjini na Manyovu