Katibu mkuu wa CHADEMA TAIFA Dk Wilbrod Peter Slaa amesema kuwa Amani, Umoja na mshikamano bila kuwa na katiba bora haiwezekani!
Akihutubia maelfu ya Wafuasi na Wanachama wa CHADEMA katika mji wa Karatu huku akiwa na Mabere Marando alisisitiza kwamba katiba bora na yenye kuleta usawa kwa watu wote ni ile inayomjali masikini na mtu mdogo katikka nchi hii na ambayo itatoa fursa kwa kila mtu kufaidi rasilimali ya nchi hii tofauti na sasa ambapo Matajiri na viongozi ndio wanaogawana rasilimali ya nchi huku watanzania walio wengi wakibaki katika umasikini wa kutupwa.
Dk Slaa aliyasema hayo leo ktk muendelezo wa mikutano inayofanywa na chama cha CHADEMA kutafuta maoni ya wananchi juu ya rasimu ya katiba mpya.
Source; ITV habari saa 2 usiku.