Zamazamani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2008
- 1,869
- 787
Hivi kuna cheap idea zaidi ya "maisha bora kwa kila mtanzania" au "nguvu mpya, kasi mpya na sijui ari mpya". Magufuli si ndio alikuwa anasimamia hayo. Au hilo leo mnamsukumia muungwana tu?
Litawezekana kama watafuata ushauri aliowaambia wananchi - Wawachague wabunge wa upinzani wawe wengi waweze kupiga kura za kutosha ya kubadilisha posho zao. Unataka aende bungeni akamshawishi nani? hao mafisadi yaliyoshinda ubunge mwaka 2005 kwa kutugaia fulana za epa, na sukari za tangold na khanga za meremeta. hao wanaojua sasa deep green sio as deep as it used to be. 2010 pesa watatoa wapi? Atakayemtolea macho mwenzake atakuwa nani?
Dk Silaha piga nondo kama kawaida mpaka wakuelewe. Unachoongea wengi hawakipati wanaelea tu. Hamna wazo la zamani au jipya hapa. Kama issue inatusumbua hata iwe ya zamani kiasi gani kama bado machungu yake tunayasikia tupige kelele.
Kama ni wazo la zamani inamaanisha ndo halifai? Mkama, wananchi gani wnapitisha posho ya Wabunge? Labda ni wananchi wa Jimbo lenu na kama ni wao basi nyote ni wajinga! Nijuavyo mimi ni Wabunge wenyewe ndiyo hupigania maslahi yao pale Bungeni wakidai waongezewe posho na mishahara na sisi wananchi wenye akili (labda wewe si mmoja wetu) hupingana na mawazo ya kuwaongezea posho wabunge kwa hiyo ni Wabunge wachache sana (kama Dr Slaa) hupingana na mawazo ya Wabunge wenzao katika suala la posho.
Inawezekana kuwa Dk ametoa cheap idea, lakini haina maana kuwa kwa kuwa ni cheap basi siyo point! Inaweza kuwa cheap idea but strong one. Jambo hilo haliwezi kutokea Bungeni kwa Wabunge ambao wewe unadai alipeleke huko akawatolee macho Wabunge wenzake ambao hawawezi kumuunga si mguu tu bali hata kidole! Ni bora atuletee wapiga kura ambao tunaweza kuwakomalia hao Wabung mwakani kupitia kura zetu.
Huu ni unafiki tu... Na utaendelea kuwa unafiki iwapo ataendelea kupita mitaani na Sangara wake akijinadi kwa posho la wabunge. Zaidi nitafurahi iwapo nitamsikia bungeni akilikoromea hili kama anavyofanya kwa issue zingine.Dk Slaa alisema suala hilo amekuwa akilipigia kelele kila wakati, lakini kutokana na kuwepo na wabunge wengi wenye ubinafsi, suala hilo limekuwa likipingwa na hivyo kuwataka wananchi kubadilika na kuchagua wabunge wengi wa upinzani, ili kuongeza nguvu bungeni na kusaidia kulinda malislahi ya nchi.