BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Date::3/16/2009
Dk Slaa kuishikia bango kampuni ya Deep Green Bungeni kwa ufisadi
Na Mussa Juma, Moshi
Mwananchi
Dk Slaa kuishikia bango kampuni ya Deep Green Bungeni kwa ufisadi
Na Mussa Juma, Moshi
Mwananchi
MBUNGE wa jimbo la Karatu, Dk Wilbrod Slaa amesema anakusudia kuwasilisha hoja binafsi kwenye mkutano ujao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kulitaka kuunda kamati maalum ya kuichunguza kampuni ya Deep Green Finance Ltd ambayo inahusika na ufisadi wa zaidi ya Sh10 bilioni za umma.
Mwaka juzi, Chadema ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikidai kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliilipa kampuni hiyo jumla ya Sh10,484,005.39/- katika mazingira yaliyojaa utata yaliyofanyika kati ya Agosti 1 na Desemba 10, 2005.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hakukuwepo na shughuli nyingine hadi Deep Green ilipoomba kutangazwa mufilisi.
Juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kimanganuni, Kata ya Uru Mawela, Dk Slaa alidai kuwa kampuni hiyo kwa kushirikiana na benki moja ya Afrika Kusini iitwayo Ned Bank inatuhumiwa kuhusika kwenye ufisadi wa fedha hizo za umma na hivyo ni lazima uchunguzwe na bunge kwani kuna ushahidi mkubwa ambao umepatikana hivi sasa.
Alisema hivi sasa serikali ya Afrika Kusini imeanza uchunguzi juu ya wahusika wa Ned Bank ambao walishirikiana na Deep Green kuchota fedha hizo kutoka BoT.
Nitapeleka tena hoja hii bungeni... kama ikikataliwa tutalipeleka suala hili kwa wananchi na kueleza kwa kina na wao watachukua hatua. Ni aibu hivi sasa serikali ya Afrika Kusini kuchunguza suala hili wakati Tanzania limeachwa, alisema Dk Slaa.
Alidai kampuni hiyo ilianzishwa Machi 18, 2004, ikiwa ni takriban mwaka mmoja kabla ya kuchota fedha hizo katika mazingira ya kutatanisha. Kwa mujibu wa Taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakurugenzi wa Deep Green Finance walikuwa ni bwana Mark Ross Weston, ambaye ni raia wa New Zealand; Anton Taljaard wa Afrika Kusini na Rudolph van Schalkwyk pia wa Afrika Kusini.
Alidai wote watatu ni wakazi wa Afrika Kusini na kwamba wanaonekana kuwa ni maafisa au wafanyakazi wa Nedbank Ltd ya Afrika Kusini.
Dk Slaa alisema inashangaza kuwa kampuni hiyo iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti bila ya kuingiza hata senti moja kwa zaidi ya mwaka mmoja kuanzia Mei 1, 2004 hadi Julai 31, 2005.
Alisema uchunguzi uliofanywa na Chadema kwa kupitia nyaraka mbalimbali hususan rekodi za kibenki, ulibaini kuwa jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 ziliingizwa katika akaunti ya Deep Green Finance katika kipindi cha miezi minne tu.
Fedha zote hizo ziliingizwa katika akaunti ya Deep Green Finance, katika kipindi cha miezi minne tu, kati ya tarehe 1 Agosti na 10 Disemba 2005," alidai.
"Hiki kilikuwa ni kipindi cha mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 14, 2005.
Ni muhimu kurudia kwamba kwa ushahidi huu wa nyaraka za kibenki, kampuni ya Deep Green Finance haikuwa na hata senti moja kabla ya tarehe 1 Agosti 2005 na wala haikupokea hata senti tano baada ya tarehe 10 Desemba 2005.
Dk Slaa ambaye pia ni mbunge wa Chademaalisema chama hicho hakiwezi kukaa kimya wakati nchi inatafunwa na watu wachache huku maisha ya wananchi yakiendelea kuwa magumu.