Elections 2010 Dk. Slaa mwanamume!

Mimi nina kila sababu ya kujivunia kwa hatua tuliyofikia hadi sasa. Kusema ukweli hadi sasa tumefanya vizuri sana. Siwezi kusema kuwa tumeshindwa hadi sasa. majimbo yote ambayo mpaka sasa hayajatangazwa tuelewe kuwa hali ni tete kwa ndugu zetu wa kijani. Moja tu ambalo natamani kuliona ni 2015. Tunaenda kufanya historia hata kama sitokuwepo ila kuna watu wataandika historia hiyo. Take it from me 2015 ni mwisho wa utawala wa watu wa kijani. No matter kuwa ni chama gani kitachukua nchi ila moyo wangu unanituma kuwa wakati umewadia sasa kwa nchi hii kuandika historia na hii ndiyo inayotokea.
Changamoto kuu sasa baada ya uchaguzi huu (kama uchakachuaji utapata fursa) basi wito wangu ni kwa vyama vyote vya siasa kukaa chini na kuacha ubinafsi ili tuweze kujenga umoja wa upinzani. Chonde chonde hebu tukae meza moja na kujua twataka nini ili tuweze kuikomboa nchi hii nzuri yenye kila kitu.

Kumbuka ule wimbo mzuri
Tazama ramani utaona nchi nzuriiiiiiiiiiii
yenye mito mingi na mabonde mengi ya nafakaaaaaaaaaaaa

Mungu ibariki Tanzania
 
Asante Boramaisha, nakuunga mkono na mguu kwa yote uliyotangulia kuyasema, Dr Slaa ametufanya kuona kwamba Tanzania bado kunamatumaini ya utaifa wa kweli tuliokuwa nao baada ya uhuru na miaka ya mwanzo ya ccm, ila wachache kwa kutumia ccm wakafanya kama vile uongozi wa nchi hii ni wa kwao na watu wao, yalishatokea mengi na wananchi wameweza kuyavumilia kwa sababu tuu waliamini kuwa bado kuna watu kwenye uongozi wana mtazamo wa kizalendo wa kitaifa na kwa maana hiyo walikua wanaiamini ccm kama mkombozi wao ila kwa ujinga wa ccm wa kujisahau na kuanza kuibia taifa letu bila aibu na kwa nguvu wakilazimisha uporaji wa mali za nchi hii waziwazi raia wamepata mwamko wa wazi baada ya mkombozi wetu Dr Slaa kusimama kidete kudai haki za mtanzania na mali za nchi yake bila kuogopa vitisho vya ccm baada ya kuzunguka nchi nzima akizungumza kifua mbele bila uoga sasa tunaona matokeo ya mwamko wa kiraia juu ya nchi yetu Tanzania kwa wapenda haki, Dr Slaa ni shujaa wetu wa kipindi hiki na tunamheshimu sana kwa kujitolea kwake kuamsha hisia za watanzania kudai haki zao kwa nguvu zote na tutaendelea kumkubali kama mwanamageuzi wetu kiongozi wa kipindi hiki kama shujaa wetu mwaminifu aliyesimama mbele ya mafedhuli na maadui wa maendeleo ya nchi yetu, saluti sana jemedari wetu Dr W P Slaa. tumeshinda sanaaaa uchaguzi huu na tunajivunia sanaa kwa hili. Hongera sana Raisi wetu tuliekuchagua Dr Slaa. Amani iwe kwetu Tanzania.
 
hata kama kitwete atarudi tena magogoni lkn mimi binafsi raisi wangu atakuwa mh. W P Slaa kwangu yeye ni zaidi ya kiongozi.
lkn bado tuna nafasi ya kushinda, na tutashinda tu.
naamini huko alikuko lazima atakuja ni kitu kikubwa sana.
Mungu bariki hiki kipenzi cha watanzania
 

Tunashukuru zaidi kwa misimamo dhabiti ya CHADEMA kutokuwachukua watu waliolifedhehesha taifa hili Kiufisadi na Uongozi mbovu kuwa wanachama wa CHADEMA. Tunashukuru zaidi kwa Kutambua kuwa kuna umuhimu wa kuwaamini na kuwapa Ujasiri Vijana kuijiunga na CHADEMA. Huu ndio msingi wa Taifa letu lijalo.

Hongera Dr. Slaa na timu yako ya Uongozi wa CHADEMA. Tuko Nyuma yenu katika kutuelekeza kuwa kazi ya CCM ilikuwa ni kuleta Uhuru; kazi ya Ujenzi wa Taifa imara lenye maisha bora kwa watu wake na Kujitegemea kwa kila Kitu ni la CHADEMA. AMEN
 


Nakuhakikishia hatakuja kushinda. Kosa halitafanyika tena! Upinzani labda 2010!
 
Mkuu, nakushauri uombe safu ya kurasa japo moja Mwanahalisi au Rai(sidhsni kama Muhingo ataruhusu itoke) lakini kiukweli Slaa KAMFUKUZISHA KAZI MAKAMBA, subirini muone....
 
Mkuu, nakushauri uombe safu ya kurasa japo moja Mwanahalisi au Rai(sidhsni kama Muhingo ataruhusu itoke) lakini kiukweli Slaa KAMFUKUZISHA KAZI MAKAMBA, subirini muone....

Mkuu MzittiKabwela Vipi Segerea?
 

hapo niaje kwani matokeo yaonesha kashindwa? au utangulizi kunipima akili zangu??
umeandika vyema lakini ungechukulia kama itatokea kama atashindwa
na si kuchukulia kuwa ameshindwa
 
Nami pia napenda kuungana na wewe kumpa Dr. Slaa pongezi za dhati kwasababu amewashikisha adabu CCM na kwamba kutokana na yeye kugombea uraisi na kura alizopata natagemea CCM watajifunza. Ingawa sera zake zingine sikubaliani nazo. Lakini kawashikisha adabu CCM.
 
Watu msikate tamaa, kamba hukatikia pabovu. Avumaye baharini papa kumbe wengine wapo ! Hakuna vita tamu ya kupigana kama unajua mapema mbinu za adui wako na alivyojipanga. Mzoea vya kunyonga, vya kuchinja ataviweza ? Heko Chadema, nawavulia kofia na kweli kamanda mnaye ! Mjinga huonyesha karata zake mapema na kwa hilo wapinzani wenu wakubwa wametia fora ! Uchaguzi huu ulikuwa wa wananchi kuamua kama wanataka mwanga au giza, wanataka uadilifu au uhuni, wanataka uongozi au usanii, wanataka uaminifu au ulaghai, wanataka ukweli au uongo, wanataka wema au ubaya na wanataka maendeleo au kinyume chake - mbona hapo jibu liko wazi ? Well, wananchi wameamua na hakuna nguvu, risasi, mabomu, wizi, vitisho, uchakachuaji, unafiki, ufisadi au aina yoyote ya uovu utakaobatilisha maamuzi yao. Hapo CCM imeula wa chuya, Kikwete atakwenda na maji !
 
Tatizo lenu mnahubiri makanisani ndo maana hamkupata kura sehemu nyingi ambazo hakuna makanisa. tunajua kuwa mlitangazwa sana na vyombo vya habari kwa sababu vingi ni vyenu lakini mpaka sasa hivi nikiamgalia matokeo sioni tofauti ya aliyetangazwa sana (Slaa) na ambaye hakupigiwa debe sana (Lipumba). And this ia shame.
Napendekeza yafuatayo;
.toeni kampeni zenu makanisani kuja viwanjani kwani sio wote wapiga kura ni wana kanisa
.ongeeni na wenzenu wa CUF ikiwezekana muunganishe nguvu
.badilisheni tabia yenu ya kujichagua wakristo peke yenu mpaka hata sehemu walipo waislam wengi mnasimamisha wakristo
.toane ufamilia kwenye chama, mfano, mbowe na mkwe wake mtei, ndesa na watoto/wakwe wake kupeana ubunge wa viti maalumu wakati hata huko Tarime ambako walipata kura nyingi hawajapewa nafasi
OTHERWISE 2015 YOU ARE FINISHED. MTASHINDA KWENYE WAKRISTO WENGI TU TENA WALE WANAOTAKA SHARI, na hata wale wasiotaka shari hawatawapigia kura kama walivyofanya mwaka huu.
 
Mapambano ya ukombozi dhidi ya CCM ndo yameanza. Huu moto hakuna wa kuuzima hadi kieleweke. Hakuna kulala hata huko bungeni, this time watajua kuwa Ukombozi baaaaado mbichi. Hapo ni kama kisamvu ndo kimepandwa, sasa kikija kukua, kuvunwa na kutwangwa mmmh.......utamuuliza Makamba atakwambia.
 
nani kakwambieni kuwa Dr. Slaa Kashindwa?
 
Ni Kweli tunastahili kumpongeza Dr kwa ushujaa wake, ashinde, ashindwe heshima yake iko pale pale, ni sauti yake imabadilisha watanzania waliokuwa bado wanasinzia, ni sauti yake iliyoengeza kura nyingi za wabunge wa chadema kutosha,
Sio kukata tamaa ni ukweli kwamba kura hazitatosha this time, na wala sio kwa kuchakatuliwa, ni za kweli watu wamepiga hivyo, tusijidanganye ila tukubali ukweli huu kwamba, watanzania wengi, hasa wa vijijini walikuwa bado hawajaguswa na mabadiliko, kwa maana hio ni sisi jukumu letu la kuendeleza mpaqmbano toka muda huu kuweka somo lisomeke 2015, tusichakatue mambo ila tuende na ukweli huu, tuelimishe waliolala na hasa ndugu zetu vijijini na wale sugu wa mjini.
Tuandae party ya kitaifa kwa ajili ya kumpongeza Dr kwa heshima kubwa ya kulibadili bunge la Tanzania lijalo. Mungu amjalie afya tuzidi kujipanga.
 

Hakuna uchaguzi ambao CCM waliwahi kulala usingizi. Labda Chadema walikuwa wamelala chaguzi zilizopita na uchaguzi huu ndiyo wameamka. Tusidanganyane hapa! Kilichotokea ni kurudia kile alichofanya Lyatonga Mrema. Hakuna jipya kwani idadi ya viti vya Chadema haifiki hata nusu ya robo ya viti vyote vya kuchaguliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…