Wakati wanaondoka Bungeni, Rais Kikwete alikatiza hotuba yake, akanyamaza huku uso wake ukisononeka; akawa ameduwaa, akakohoa kidogo, huku wabunge wa CCM wakipiga makofi kuwazomea CHADEMA; na baadaye alitoa kauli ya kejeli akisema, Hata wasionichagua hawana serikali nyingine ni hiihii. Watakwenda, watarudi, hawana mwingine wa kumwomba yao yatimie zaidi ya serikali ya CCM ambayo mie ndiye rais wake.