- Feb 10, 2006
- 4,324
- 13,967
Imeandikwa na Tumaini Msowoya, Iringa na Brandy Nelson, Mbeya
Mwananchi
August 3, 2010
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema, Willibrod Slaa jana aliendelea kuvuta watu wengi kwenye mikutano yake mjini Mbeya na Iringa ambako aliwaeleza wananchi kuwa ameinasa barua kutoka makao makuu ya CCM kwenda kwa wakuu wa wilaya ikiwataka kuwakusanya wafanyabiashara katika maeneo yao ili wawachangie fedha kwa ajili ya kampeni za chama hicho.
Dk Slaa alikuwa mjini Iringa na Mbeya kusaka wadhamini baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kwa tiketi ya Chadema, alikumbana na tatizo la kunyimwa kutumia Uwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa baada ya Jeshi la Polisi kuelezwa kuwa sehemu hiyo itatumika kwa ajili ya shughuli za mbio za mwenge na baadaye mchana kuzuiwa na CCm kutumia Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Akihutubia umati wa wakazi wa manispaa ya Iringa waliofurika kwenye viwanja hivyo, Dk Slaa alisema barua hiyo ameinasa wakati ikienda kwa wakuu wa wilaya.
Huu ni wizi wa mchana, tena kweupe," alisema mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Karatu. "Hili limeniumiza sana... (hii barua) inawasihi wafanyabishara wawachangie fedha kwa ajili ya kampeni. Hili limeniumiza sana.
Alisema kuwa ni vyema michango hiyo ingekuwa ikichangishwa kwa ajili ya kuinua maisha ya Watanzania ambao wamekuwa wakiishi maisha duni tofauti na falsafa ya maisha bora kwa kila Mtanzania.
Kuhusu wafanyakazi, Dk Slaa aliibeza kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba hahitaji kura zaidi ya laki 300,000 za wafanyakazi nchini ambao waliitisha mgomo kuishinikiza serikali kuongeza kima cha chini cha mshahara na madai mengine wanayostahili.
Simtukani ila yeye mwenyewe kwa kinywa chake alisema hahitaji kura za wafanyakazi. Mimi nazihitaji sana kwani hawa ni wavujajasho wanaonyonywa huku watu wengine wakineemeka, mfano mzuri ni walimu wa shule za msingi ambao hulipwa Sh160,000 tu, alisema.
Alieleza kuwa kwa siku mbunge amekuwa akilipwa kiasi cha Sh160,000 kila akiwa bungeni wakati kiwango hicho cha fedha ndicho hulipwa mfanyakazi kwa mwezi na kukielezea kitendo hicho kuwa ni sawa na unyonyaji.
Walisema maisha bora kwa kila Mtanzania; maisha gani bora ambayo yamepandisha bei ya vitu huku kiwango cha mshahara kikiendelea kuwa kile kile? Bila huyo mwalimu ambaye amenifanya leo hii niitwe Dk Slaa, sidhani kama ningesimama mbele yenu, alisema.
Mgombea huyo aliitumia nafasi hiyo kumtangaza mwenyekiti wa wilaya ya Iringa Mjini, Dk Peter Msigwa kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge wa jimbo hilo.
Mjini Mbeya, umati wa watu ulianza kufurika Uwanja wa Ndege kuanzia saa 8:00 mchana na wakati akiwasili helikopta iliyomchukua ilizunguka angani maeneo ya mjini Mbeya, kitendo kilichokusanya watu wengi kabla ya kutua.
Baada ya Dk Slaa kupewa nafasi ya kuongea, alieleza jinsi
alivyosikitishwa na kitendo poilisi kuizuia Chadema kutumia uwanja huo kama ilivyokuwa mjini Iringa.
Unajua kuna watu ambao wanadhani hii nchi ni mali yao peke yao," alisema. "Nimesikitishwa sana na tabia ya CCM kutunyima Uwanja wa Sokoine kufanya mkutano wakati viwanja hivi ni mali za wananchi wote kwa kuwa vilijengwa wakati wa kipindi cha chama kimoja."
Alisema kuwa Chadema haitavumilia kitendo hicho na kwamba endapo kama chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi kitanyang`anya viwanja vyote na kuwa ni mali ya Watanzania wote.
Dr Slaa pia aliwashambulia polisi na kuwataka kuacha mara moja kufanya mchezo wa kuisaidia CCM katika uchaguzi mkuu ujao.
Nawatahadhalisha kabisa msije mkapata matatizo... muache mchezo wenu wa kuisaidia CCM katika uchauzi mkuu. Mkitaka kufanya hivyo, mvue magwanda yetu muingie kwenye shughuli za Kisiasa
Kuhusu uamuzi wa kugombea urais badala ya ubunge. Dk Slaa alisema kitendo cha wananchi kujitokeza kwa wingi kinamfanya aamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyempa ufahamu wa kufanya hivyo.
Akiwa mjini Iringa, Dk Slaa pia alipinga vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kumzuia kutumia Uwanja wa Mwembetogwa wa mjini Iringa kwa madai ya shughuli za mwenge.
Sisi tumeomba uwanja saa 4:00 asubuhi, cha ajabu polisi wanazuia uwanja huu tusiutumie ili kuuachia nafasi mwenge ambao unawasili saa 8:00 mchana kwa ajili ya kuzindua mradi. Hii maana yake nini? Au wanataka tufanyie mikutano angani? Polisi hawana mamlaka ya kuzuia matumizi ya uwanja kwa ajili ya kampeni. Nawashukuru viongozi wangu kwa kuamua kuufanyia mkutano huu hapahapa tena kwa mabavu, alisema Dk Slaa.