Lunyungu,
Wewe mwaga data tu, nilishawahi kusema kuwa kabla ya Oktoba tutayaona na kuyasikia mengi.
Lunyungu,
Asante sana kwa kunimegea Taarifa kuhusu njama za CCM mkoa wa Arusha.
Ni kweli nimepata Taarifa hizo. Zinatokana na ukaguzi wa Bodi ya Maji ya Vijiji sita vya Karatu mjini na Vitongoji vyake inayoitwa Bodi ya Kaviwasu. Bodi hiyo imekuwa ikikaguliwa na Wakaguzi wa nje toka mwaka 2001 kama sikosei. Hivi Karibuni kulikuwa na malalamiko, na mimi mwenyewe hadharani nikamwagiza Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye kwa mujibu wa Sera ya Wilaya Halmashauri yake ndiyo Regulatory authority waikague Body hiyo.
Kwa bahati mbaya badala ya kuwaita wakaguzi wenye sifa, wakatuma Internal Auditor na maafisa Ushirika kuikagua Bodi hiyo. Mimi nikawaeleza kuwa kwa utaratibu iwapo chombo kimekaguliwa hakiwezi kukaguliwa na wakaguzi wasio na Sifa ( Internal auditor wetu aliisha kukataliwa mahakamani kwa kutokuwa na sifa na Halmashauri ikapoteza kesi). Kimsingi wakaguzi hao walifanya ukaguzi wao, ambao kwa vigezo vyote hauna sifa, wakatoa taarifa kuwa Bodi hiyo imetafuna jumla ya Tshs 400 Millioni. CCM wakadakia hoja hiyo ambayo ilikuwa ikijadiliwa katika ngazi ya Halmashauri ya Wilaya.
Ili waweze kumchafua Dr. Slaa watakuwa na kazi kubwa:
i) Kwanza Dr. Slaa siyo mjumbe kwenye Bodi ya Kaviwasu, japo Bodi zote 7 za Maji Wilayani Karatu nilizianzisha mimi, na Katiba zao niliziandika mimi kwa mkono wangu kwa kushirikiana na Wizara ya Maji, wakati ule Bwana Kobalyenda.
ii) Ili mtu uchafuliwe ni lazima waonyeshe kuwa tarehe fulani ulichukua fedha kiasi fulani, na kadhalika. Bila kuonyesha hilo itabaki propaganda kama inavopigwa propaganda na ccm katika mambo mengi. Wananchi wa Karatu ndio wanaojua Dr. Slaa na Kaviwasu wakoje.
Itawageuka vibaya, ni vyema waje nayo kama walivyokuja na fedha za Kanisa na za Walemavu na hazikuwapeleka popote. Mimi ninawakaribisha sana. Hata hivyo asante sana, kwa Taarifa na kwa mapenzi ya dhati kwangu. Mungu awabariki.