Dk.Slaa unajua kwamba CCM Arusha wanakuundia kashfa nzito?

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
8,873
Reaction score
1,906
Mh.Dk Slaa rafiki wa watanzania wote wakiwemo wana CCM wasafi na kuacha wachache wachafu na wasio na heshima wala upendo na Tanzania yangu , CCM Arusha wanakuundia kashfa nzito ili waweze kuitumia dhidi yako kwenye kampeni za Oct 2010. Wana dai umekula pesa ya mradi wa maji katika Jimbo yapata sh.400mn za Kitanzania n a mengine mengi. Haya ndiyo yanayo jiri sasa na wanajipanga kweli baada ya kushindwa kusema juu kashfa nyingine ya misaada ya Kanisa. Sasa kama ulikuwa hujui basi amka fuatilia na kama ulikuwa unajua basi kaza buti mambo si mambo Mzee wetu CCM fitina na wao wanataka madaraka na si ustawi wa Tanzania .Kuna mkono wa mwenyekiti wao na hivyo jungu ni kubwa mno na wana hasira umewabwaga Mahakamani pia .

Nitasema mengine na kuweka data zaidi kadiri wanavyo zidi kuji zatiti .
 
Lunyungu,
Wewe mwaga data tu, nilishawahi kusema kuwa kabla ya Oktoba tutayaona na kuyasikia mengi.
 
Lunyungu,
Wewe mwaga data tu, nilishawahi kusema kuwa kabla ya Oktoba tutayaona na kuyasikia mengi.
Lunyungu,

Asante sana kwa kunimegea Taarifa kuhusu njama za CCM mkoa wa Arusha.

Ni kweli nimepata Taarifa hizo. Zinatokana na ukaguzi wa Bodi ya Maji ya Vijiji sita vya Karatu mjini na Vitongoji vyake inayoitwa Bodi ya Kaviwasu. Bodi hiyo imekuwa ikikaguliwa na Wakaguzi wa nje toka mwaka 2001 kama sikosei. Hivi Karibuni kulikuwa na malalamiko, na mimi mwenyewe hadharani nikamwagiza Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye kwa mujibu wa Sera ya Wilaya Halmashauri yake ndiyo Regulatory authority waikague Body hiyo.

Kwa bahati mbaya badala ya kuwaita wakaguzi wenye sifa, wakatuma Internal Auditor na maafisa Ushirika kuikagua Bodi hiyo. Mimi nikawaeleza kuwa kwa utaratibu iwapo chombo kimekaguliwa hakiwezi kukaguliwa na wakaguzi wasio na Sifa ( Internal auditor wetu aliisha kukataliwa mahakamani kwa kutokuwa na sifa na Halmashauri ikapoteza kesi). Kimsingi wakaguzi hao walifanya ukaguzi wao, ambao kwa vigezo vyote hauna sifa, wakatoa taarifa kuwa Bodi hiyo imetafuna jumla ya Tshs 400 Millioni. CCM wakadakia hoja hiyo ambayo ilikuwa ikijadiliwa katika ngazi ya Halmashauri ya Wilaya.

Ili waweze kumchafua Dr. Slaa watakuwa na kazi kubwa:

i) Kwanza Dr. Slaa siyo mjumbe kwenye Bodi ya Kaviwasu, japo Bodi zote 7 za Maji Wilayani Karatu nilizianzisha mimi, na Katiba zao niliziandika mimi kwa mkono wangu kwa kushirikiana na Wizara ya Maji, wakati ule Bwana Kobalyenda.
ii) Ili mtu uchafuliwe ni lazima waonyeshe kuwa tarehe fulani ulichukua fedha kiasi fulani, na kadhalika. Bila kuonyesha hilo itabaki propaganda kama inavopigwa propaganda na ccm katika mambo mengi. Wananchi wa Karatu ndio wanaojua Dr. Slaa na Kaviwasu wakoje.

Itawageuka vibaya, ni vyema waje nayo kama walivyokuja na fedha za Kanisa na za Walemavu na hazikuwapeleka popote. Mimi ninawakaribisha sana. Hata hivyo asante sana, kwa Taarifa na kwa mapenzi ya dhati kwangu. Mungu awabariki.
 
Tunakuamini sana Mkuu wetu na pia kama wanataka kuelta ushetani wao basi watashindwa na kusambaratika kabisa. Mungu yupo pamoja na wewe
 
hawajaanza leo kwa iyo hakuna jipya
 
Yaani hawajaridhika na tape recorder waliyoitega kule Dodoma?
 
Mkuu watasema mengi sana, lakini mimi nawaambia kelele za chura na za mpangaji dhidi ya ngombe na mwenye nyumba hazitafua dafu, na hilo naita debe tupu kwani jadi yake haliachi kutika (No evidence/data). Mbulu tuna bora mbunge tunamtafuta mbunge bora 2010 pindi piriton waliyomeza wapiga kura wengi kuisha nguvu, huku sisi weledi tukijaribu kuwaponya na kuhakikisha hawapewi nyingine. Fools bite one another, wise men agree together.
 
Lunyungu,
Wewe mwaga data tu, nilishawahi kusema kuwa kabla ya Oktoba tutayaona na kuyasikia mengi.


Mzee Jasusi mimi niko nao hawa na nashukuru kama Dr.Slaa kalijua hili .Nitasema mengi kadiri tutakavyo kuwa tuna maliza vikao .Sitakaa kimya kabisa .
 
Hawa CCM....sasa nasikia wanafanya harambee ya kuchanga 500m kumng'oa Ndesamburo Moshi waurudishe mji ule nyuma....hizo hela zinaweza kufanya mengi kwa jamii kuliko kumng'oa Ndesa.....I wish tungekuwa na majisiri wa kisiasa wa kutosha kama hawa wazee wawili...Slaa na Ndesa...Sadly ndani ya CCM wapo lakini huo ujasiri wa kutoka na kujiunga na haya magwiji ndio ukoma wenyewe...
 

CCM laana tupu . Hizo pesa zaweza kuliwa na Ndesa akarudi Bungeni tena . Watu wa Moshi ndiyo wanajua nini Ndesa kafanya na kule Karatu CCM wao kila siku ni pesa kutembeza tu .
 
CCM laana tupu . Hizo pesa zaweza kuliwa na Ndesa akarudi Bungeni tena . Watu wa Moshi ndiyo wanajua nini Ndesa kafanya na kule Karatu CCM wao kila siku ni pesa kutembeza tu .

Hii awareness ingeenea nchi nzima ingekuwa safi sana...
 
Mheshimiwa Dr. Slaa,
Naamini zengwe hili si lako binafsi ila ni kwa upinzani na hasa Chama chako cha Chadema.
Wanataka kuonyesha kuwa hamuwezi uongozi kwani halmashauri ya Karatu iko chini ya Chadema.
Naomba litizame kwa mnasaba huo zaidi.
 
Dr Slaa,
Mbona siwasikii kuhimiza wapiga kura kujiandikisha?Naogopa kuwa hawa wananchi wanaojitokeza katika mikutano yenu hatimaye hawapigi kura....CCM inahimiza watu wao kimyakimya vipi nyie CHADEMA?
 
Nisha wahi sema na kurudia tena kwanini CCM wao waweke mikakati ya kukusanya pesa nyingi ili kumng'oa mtu mmoja katika jimbo fulani ili hali wakijua kuwa wananchi wa jimbo hilo wanamtambua mgombea wao ndio huyo huyo na ndie wanaeridhika nae na kweli ukitizama kuna maendeleo katika hilo jimbo sasa wao CCM kwanini wasije na sera zao mpya tuu na kijitahidi kufanya kazi na mtu wa upinzani na ndipo maendeleo huanzia na huwezi jua huko baaadae hao hao viongozi wanaweza kubariana na kuachiana madaraka kila muhura wa uchaguzi ujapo.

Lakini kukaaa chini na kuwekeana fitna na shutma mbali mbali sio sawa ina dhihirisha wazi kuwa CCM hamjakomaa kisiasa swafi bali mpo kupiga domo tuu na tena nasio kwa maslahi ya wananchi bali ni kwa maslahi yenu viongozi wachache, jamani tubadilike kihoja hapa na sio fitna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…