LGE2024 Dkt. Ananilea Nkya: Wanawake jitokezeni kuwania nafasi za Uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Dkt. Ananilea Nkya: Wanawake jitokezeni kuwania nafasi za Uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Ikiwa zimebakia siku chache kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini, Dk Ananilea Nkya amasema kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo upelekea Wanawake kushindwa kuwania na kuchaguliwa kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Ametolea mfano kuwa moja wapo ni 'changamoto ya Kikatiba', ambapo amedai kwamba wamekuwa wakipigania kudolewa Viti maalumu ili kuondoa utamaduni ambao amedai kuwa unawalemaza baadhi ya Wanawake kuamini kwamba nafasi hiyo ndio fursa inayoweza kuwafanya wakapata nafasi za Uongozi kirahisi.

Amedai kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa haitoi nafasi ya Viti maalumu kwa Uwenyekiti wa Mtaa, Vijiji wala Vitongoji. Amesema kuwa Wanawake wanatakiwa kuamka kuwania nafasi kwa kuingia kwenye kinyanganyiro kwa kuwa ngazi hizo za uongozi ndio fursa ya awali ambayo inawezesha kuzungumza changamoto zao.

Aidha amesema kuwa vyombo vya habari havilipoti habari za Uongozi kwa mwendelezo hali ambayo amesema kuwa ingeweza kubadili utamaduni uliojengeka kuhusu Uongozi.

"Vyombo vyetu vya habari viko chini katika kuripoti ya Uongozi na kusaidia jamii iamke, waandishi wa habari, vyombo vya habari vinazungumzia masuala ya Uongozi miezi kadhaa kabla ya uchaguzi, wakati Uongozi ni suala la kila siku tunatakiwa tuyazungumze.

Anaongeza "Lakini hata kuandika story za Uongozi waandishi wengi hawajui"

Itakumbukwa kwa mujibu wa ripoti ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, Wanawake ambao walifanikiwa kupata nafasi ya kuwa Wenyeviti wa Vijiji nchini ni asilimia mbili, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa 13 na asilimia saba Wenyeviti wa Vitongoji Vitongoji.
 
Back
Top Bottom