- Source #1
- View Source #1
Wakuu salaam,
Nimekutana na posti hii ikielezea kuwa Anna Henga wa LHRC wamesema kuwa CCM kuuawa ni haki yako huku ikiwa na picha ya yule Mama wa CCM aliyeuawa hivi karibuni.
Post hii hapa Chini:
Nimekutana na posti hii ikielezea kuwa Anna Henga wa LHRC wamesema kuwa CCM kuuawa ni haki yako huku ikiwa na picha ya yule Mama wa CCM aliyeuawa hivi karibuni.
Post hii hapa Chini:
- Tunachokijua
- Dkt. Anna Henga ni mtetezi wa haki za binadamu na mwanasheria mashuhuri kutoka Tanzania. Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Kumeibuka 'Post' yenye Nembo ya Watetezi TV inayodai Dkt. Anna Henga amesema "CCM kuuawa ni haki yao", Post hiyo imeambatanishwa picha Dkt. Anna (kushoto) na Christina Kibiki aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo aliyeuawa usiku wa kuamkia November 13, 2024 (taarifa za kifo chake zipo hapa).
Upi uhalisia wa 'Posti' hiyo?
Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Post hiyo haina ukweli na imetumia nembo ya Watetezi TV ili kupotosha.
Kuhusu chapisho na Nembo ya Watetezi TV?
Uchambuzi wa kimtandao JamiiCheck umebaini kuwa Taarifa hiyo halijawahi kuchapishwa katika kurasa rasmi za Watetezi TV kama inavyoonekana.
Mtengenezaji wa chapisho hilo ametumia rangi zinazofanana na Watetezi TV lakini mwandiko uliotumika (Font) sio ule unaotumiwa na Watetezi katika kutoa taarifa zao nyingine.
Uhalisia wa Nukuu ya Dkt. Anna Henga?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa nukuu na kuhusishwa na Dkt. Anna imezeshwa tu na hakuitamka katika Mkutano wa LHRC na Waandishi wa Habari (Dkt. Anna akiwa mzungumzaji).
Aidha, kauli hiyo haikuwekwa kwenye barua maalumu ya Novemba 13, 2024 iliyotolewa na LHRC (tazama rejea hapa) ya kulaani mauaji ya Christina Kibiki iliyoandiwa na Dkt. Anna.