Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji amegawa pikipiki 700 na vishkwambi 4,500 kwa ajili ya matumizi ya maafisa ugani wa sekta ya mifugo mkoani Morogoro.
Dkt. Kijaji amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa na mkoani Morogoro kwa ujumla huku akihamasisha ufugaji wa kisasa.
“Rais wetu anawapenda sana wafugaji wa nchi hii na ameidhinisha Shilingi Bil. 28 kwa ajili ya uchanjaji wa mifugo yote ufanyike ili kulinda afya za walaji na kuongeza uhakika wa soko la kimataifa la nyama na mazao yake”. Ameongeza Dkt. Kijaji
Dkt. Kijaji pia amewataka maafisa ugani kufika kwenye maeneo ya vijijini kwa lengo la kuwafikia wafugaji moja kwa moja na kuwatatulia kero zinazowakabili.