Dkt. Ashatu Kijaji azindua Jengo la Mionzi katika Hosipitali ya Wilaya ya Kondoa

Dkt. Ashatu Kijaji azindua Jengo la Mionzi katika Hosipitali ya Wilaya ya Kondoa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewataka watumishi wa afya katika Halmashauri ya Kondoa pamoja na Halmashauri ya Mji Kondoa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuwa wananchi hao wanamatumaini makubwa ya kupata huduma kwa haraka na kwa uhakika.

Ameyasema hayo tarehe 29 Aprili, 2023 katika uzinduzi wa jengo la mionzi katika Hosipitali ya Wilaya ya Kondoa iliyopo Bukulu pamoja na uzinduzi wa jengo la huduma za dharura katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa.

Akizungumza kwa nyakati tofauti Mheshimiwa Waziri Kijaji amemshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini na kumpatia jukumu la kufanya uzinduzi wa majengo hayo ikiwa ni sehemu ya shughuli za wiki ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewekezeka fedha nyingi katika afya kwa lengo la kuhakikisha watu wanapoumwa wanapata matibabu kwa gharama nafuu kwenye maeneo waliyopo bila kuhitaji kwenda mbali.

Aidha, aliwataka watendaji kutokufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa Serikali haitavumilia jambo hilo. Vilevile ametoa rai kwa viongozi wanaosimamia utoaji wa huduma za afya kuhakikisha vituo hivyo vinatoa huduma bora zaidi ili viwe kimbilio kwa watu wengi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Kijaji ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya vituo vya afya na kuwapatia kibali cha ajira katika kada ya afya na ana matumIni kuwa Halmashauri hizo zitapata watumishi.

Awali, akimkaribisha Mheshimiwa Waziri, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Dk. Khamisi Kahanacho, amesema ujenzi wa jengo la Mionzi katika Hosipitali ya Halmashauri ya Kondoa na jengo la huduma za dharura katika Hospitali ya Mji Kondoa una lengo la kuboresha utoaji wa huduma za dharura pamoja na kuwezesha upimaji wa wa haraka kwa wagonjwa kwa lengo la kuboresha huduma za afya na kupunguza vifo.

Aliongeza kuwa majengo hayo yatahudumia wananchi wa Wilaya ya Kondoa na viunga vyake pamoja na Mikoa ya jirani.

WhatsApp Image 2023-04-30 at 10.41.22.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-30 at 10.41.22(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-30 at 10.41.23.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-30 at 10.41.23(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-30 at 10.41.23(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-30 at 10.41.24.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-30 at 10.41.24(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-30 at 10.41.25.jpeg
 
Back
Top Bottom