Pre GE2025 Dkt. Ave- Maria Semakafu: Viti maalumu viwe kwa ajili ya Gen-Z

Pre GE2025 Dkt. Ave- Maria Semakafu: Viti maalumu viwe kwa ajili ya Gen-Z

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mratibu wa Kitaifa wa Umoja wa Wanawake Wanasiasa (Ulingo), Dk Ave- Maria Semakafu amesema anatamani wanasiasa wanaochipukia ndio wapate ubunge wa viti maalumu ili wazoefu waende majimbo wakashindane.

“Ningetamani kuona Gen-Z (wanasiasa wanaochipukia) waende kwenye viti maalumu, sisi watu wazima wenye uzoefu twendeni moja kwa moja majimboni kupambana ili kuwapa fursa watoto,” amesema.

Amesema hayo Jumatano Machi 5, 2025 akichangia mjadala wa Mwananchi X Space uliojadili mada isemayo: “Ni sahihi kuwa na ukomo ubunge, udiwani viti maalumu” ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL).

Amesema: “Natamani sanasana kwanza hadhi ya viti maalumu ipandishwe ili kweli wanapokwenda pale wanakuwa wabunge. Huwezi kuwa mbunge, halafu huingii jimboni hadi upewe kibali na mbunge mwenye jimbo lake.

“Huyu anayeitwa viti maalumu haruhusiwi kufanya kitu chochote hadi apate kibali cha mwenye jimbo, la sivyo anajipitishapitisha. Jamani hizi siasa zimepitwa na wakati,” amesema.
 
Mbona yeye anaogopa kugombea???
Achukue form aingie ulingoni aone moto unavowaka
 
Back
Top Bottom