Dkt. Ayub Rioba: Ninachokataa ni watu kudhani shida zao zote zinasababishwa na Katiba

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha, amepinga mtazamo wa kwamba kupatikana kwa Katiba Mpya ndiyo suluhu pekee ya changamoto zote zinazoikabili nchi.

Akizungumza Julai 28, 2026, katika kipindi cha One on One cha Wasafi Media, Dkt. Rioba amesema kuwa ingawa anaunga mkono marekebisho ya Katiba ili kuendana na mabadiliko ya nyakati na changamoto za sasa, tatizo kubwa linalopuuzwa ni utamaduni na tabia za watu wenyewe, akionya kuwa hata ikiletwa Katiba bora zaidi duniani bado haitasaidia ikiwa jamii haitabadilika kifikra.

"Unajua hii katiba hata ukitizama, yaani kuna namna. Mimi sitetei kwamba lazima iwe hivyo hivyo ilivyo, Mimi nachokataa kwenye hoja yangu ni watu kudhani kwamba shida zao zote zinasababishwa na katiba eti kwamba katiba sasa hii ikisheletwa tu mpya wanayoitaka wao, ambayo inaongelea zaidi mambo ya mgawanyo wa madaraka, itatua matatizo ya nchi. Hapana."

Your browser is not able to display this video.
 
Hayo ni maoni yake. Kwasasa Tunataka KATIBA MPYA watu hawezi kubadilika kama hakuna uwajibikaji na hili linatokana na udhaifu wa KATIBA ya sasa...KATIBA ya sasa inawalinda viongozi wakubwa..Sasa kama mkubwa wako anakosea na hapewi adhabu unadhani wewe mdogo utabadilika?
 
Anasema tubadilike kifikra
 

..OCT 29 mzizi wake ni hii Katiba tuliyonayo.
 
Jamaa angeangalia afya yake kanyauka sana sijui shida nini
 
Kavimbewa huyu blaza
 
Hakuna mtu aliyesema shida zote zinasababishwa na katiba.
 
Alikua na ulaji TBC kwa kugeuza dhanq ya chombo cha habari cha taifa na kua cha chama tawala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…