Dkt. Bashiru Ally uliwahi kukiri kuwa CCM ina ombwe la viongozi. Kwanini haukemei huu uzembe?

Dkt. Bashiru Ally uliwahi kukiri kuwa CCM ina ombwe la viongozi. Kwanini haukemei huu uzembe?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Kwa wale ambao tumekuwa tunafuatilia mambo tunakumba jinsi Katibu mkuu wa Ccm alivyowahi kukiri hadharani kuwa Ccm ina tatizo la kuwa na ombwe la viongozi.

Hii ina maanisha viongozi wa CCM wapo tu ila hawajui wajibu wao kama viongozi. Ndio maana kuna shida kubwa juu ya kutatua kero za wananchi. Maana uelewa wa viongozi wengi wa CCM ni mdogo.

Katibu wa Ccm alinukuliwa akisema ndio maana Ccm imejenga chuo cha uongozi cha mwl JKN huko kibaha ili wanachama wa Ccm wawe wanaenda kupigwa msasa ili wawe viongozi bora na sio bora viongozi.

Mbona ndugu Bashiru Ally upo kimya huku wanachama wa CCM wanafanya fyongo? Wamejigeuza mamlaka za kutoa adhabu,wanatoa maagizo yasiyofaa na wewe upo kimya?

Umeshahu kuwa unatakiwa uwakemee na uwapeleke Kibaha kupigwa msasa?

Vipi kijana wako H. Polepole atawapigia simu kweye kipindi cha Papo kwa papo ili awahoji juu ya hizi fyongo wanazofanya?
 
CCM ukiwa nje ya mfumo unakuwa na akili timamu ukiingia ndani ya mfumo tu akili zinashikwa na Mwenyekiti
 
Duh,mbona mshikemshike. Vipi hiki chuo cha uongozi kinaweza kutumiwa na wapinzani? tindo ili kupata upinzani madhubuti?
 
Duh,mbona mshikemshike. Vipi hiki chuo cha uongozi kinaweza kutumiwa na wapinzani? tindo ili kupata upinzani madhubuti?

Mpinzani kwenda kwenye chuo cha CCM ni kwenda kuvikwa nadharia za ujamaa uchwara, siasa za Majungu, wizi wa kura, nidhamu za kinafiki na mauaji. Hakuna zaidi ya hilo.
 
Mpinzani kwenda kwenye chuo cha ccm ni kwenda kuvikwa nadharia za ujamaa uchwara, siasa za Majungu, wizi wa kura, nidhamu za kinafiki na mauaji. Hakuna zaidi ya hilo.
Duh. Ndugu yangu nitakujibu kesho,naona umejibu kwa gadhabu ya kukosa ushindi wa ubunge na uchaguzi mkuu.
 
Mpinzani kwenda kwenye chuo cha ccm ni kwenda kuvikwa nadharia za ujamaa uchwara, siasa za Majungu, wizi wa kura, nidhamu za kinafiki na mauaji. Hakuna zaidi ya hilo.
Kamanda, wananchi ndio walikubwaga kwenye box la kura, hivyo punguza jazba.
 
Na sasa hivi ndiyo hakuna kabisa, sijui chuo cha kuwapika hakuna!
 
Back
Top Bottom