Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru atoa onyo kwa wanaokusanya kadi za wapiga kura

Uchaguzi 2020 Dkt. Bashiru atoa onyo kwa wanaokusanya kadi za wapiga kura

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ametoa onyo kali kwa wale wote wanaopita kukusanya shadada za kupigia kura kwa visingizio vya kutoa mikopo kwa wananchi.

Ameyasema hayo leo tarehe 27, Septemba 2020 kata ya Engusero akielekea Kiteto na Mgombea Mwenza wa CCM wa Urais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan baada ya uzinduzi wa Kampeni awamu ya tatu kati ya sita, uliofanyika wilayani Kongwa mkoa wa Dodoma.

"Tusilaghaiwe, shahada yetu ya kupiga kura, ina kazi ya kupiga kura tusidanganywe kwamba shahada hiyo unaweza ukapata mikopo, ukiona mtu anakwambia hivyo mtafute mwenyekiti wa Kitongoji akamatwe na achukuliwe hatua za sheria."

Katibu Mkuu ameongeza kuwa, "Ukiona mtu anakuhamasisha kufanya fujo, usimkubalie kwasababu nchi hii ni nchi huru na ni kisiwa cha amani."

Awali, katika uzinduzi huo, Wilayani Kongwa Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuzipongeza kamati za siasa za ngazi zote pamoja na wenyeviti wa mashina kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kuhakikisha ushindi mkubwa unapatikana.

Uzinduzi huo ni wa awamu ya tatu kati ya sita ambapo awamu ya nne itafanyika Zanzibar.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 
Tume ya Uchaguzi haina hizi taarifa ? Kawe walikuwa wanatoa mkopo mpaka 500,000 sharti uwe na kadi ya mpiga kura, na wanaofanya hivyo ni wagombea wa CCM, kwanini tume isikionye CCM ama kuwaita hao wagombea kwenye tume ya maadili ?

Kuna wengine walikamatwa wakitoa rushwa wakati wa kipindi cha kura za maoni kwa Chama Cha Mapinduzi lakini Takukuru ikawaachia CCM imalizane nao , ina maana CCM ina taasisi zake ambazo zinaweza kutekeleza majukumu kwa niaba ya vyombo vya serikali ?
 
Hawa jamaa kila mtu wanamchukulia poa tu,mm nmewaambia siwezi fanya upuuzi huo
 
Tume ya Uchaguzi haina hizi taarifa ? Kawe walikuwa wanatoa mkopo mpaka 500,000 sharti uwe na kadi ya mpiga kura, na wanaofanya hivyo ni wagombea wa CCM, kwanini tume isikionye CCM ama kuwaita hao wagombea kwenye tume ya maadili ?

Kuna wengine walikamatwa wakitoa rushwa wakati wa kipindi cha kura za maoni kwa Chama Cha Mapinduzi lakini Takukuru ikawaachia CCM imalizane nao , ina maana CCM ina taasisi zake ambazo zinaweza kutekeleza majukumu kwa niaba ya vyombo vya serikali ?
Bashiru na Polepole siyo CCM kwa damu .... Hivyo hawajui kuwa hiyo ni mbinu ya siku nyingi. Unless wana mbinu ambadala awamu hii hasa baada ya Kikao cha Wakurugenzi!!
 
Hamna kitu kinanikera kama com ila hamna kitu kina nikera zaidi kama simba na yanga timu toka babu zetu wanashangilia hatuhami halafu leo tunajiita wapinzani ,tuanze na haya matimu kwanza halafu tumalize na liccm but
MAGUFULI mitano tena
 
CCM Kwa maigizo Tu wanatisha,baada ya kutosheka na manunuzi ya vitambulisho Leo ndiyo mnaanza na style ya kuzuga! Eti ni marufuku kununua vitambulisho the wakati miezi 3 yote mlikuwa mnafanya kazi ya manunuzi
 
Back
Top Bottom