Kyara Atufigwe
Senior Member
- Mar 29, 2015
- 120
- 68
Wakati wa Utawala wa Serikali ya awamu ya Tano, Dr Bashiru Ally ulikuwa Kiongozi Mwandamizi wa Chama na baadaye kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Ni imani yangu kuwa ulikuwa miongoni mwa washauri wakuu wa Serikali ya Hayati Magufuli.
Sehemu ya Ushauri wako ilipelekea Wakulima wadogo wadogo kuwa na soko baya kuliko hali ilivyo sasa. Nyanya zilikosa soko zikalishiwa ng'ombe, wakulima wa mahindi walikosa soko na mengine kuozea shambani, soko la parachichi halikueleweka, kodi nyingi za hovyo hovyo, matumizi ya mabavu n.k
Pamoja na madudu hayo yote, Dr Bashiru haukuwahi kuonekana hadharani kuwapigania Wakulima. Mara nyingi nilikuona jukwaani ukiimba nyimbo za kumsifu na hata kumuabudu aliyekuwa Mkuu wa nchi kwa wakati huo. Kwanini leo hii uone nongwa kwa Wakulima na Watanzania kwa Ujumla wanapomsifia Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuwa anafanya mageuzi makubwa nchini? Kwanini ukerwe na watu wanapoonesha hisia zao kuwa Mama anaupiga mwingi?
Dr Bashiru, Wakulima hawa hawa wadogo wadogo ambao wewe unajitahidi kupandikiza mbegu ya chuki ili Wamchukie Mhe Rais Samia na Serikali yake wana experience “boom period" katika biashara za mazao yao. Kama bei ya debe moja la mahindi wakati wewe ukiwa Katibu Mkuu wa Chama ilikuwa Tsh 4, 000/= na sasa Wakulima wanauza Mahindi kwa Tsh 20,000/= (Ongezeko la 500%)sasa kwa nini wasimpongeze Mhe Rais na Serikali yake?
Kama sasa mabavu katika kukusanya kodi hayapo tena, masoko yanazidi kufunguka, utekaji tekaji watu haupo tena amani inatawala nchini, hao hao wakulima wanalima kwa amani kabisa na mbolea ya bei ya ruzuku wanaletewa hadi vijijini, kwanini Watanzania Wasimpongeze Mhe Rais na Serikali yake?
Daima Chanda Chema huvikwa Pete. Watanzania wana kila sababu ya kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya awamu ya sita kwa ujumla kwa Transformation kubwa kwa Taifa letu. Kauli zako za chuki, husda na Wivu kamwe hazitofanikiwa. Mbegu ya Chuki unayojaribu kuipanda kwa Wakulima na Watanzania dhidi ya Mhe Rais kamwe haitoota, haitomea. Ulipata fursa ya kuhudumu katika Chama na Serikali iliyopita, sasa ni wakati wa Mama Samia na Serikali yake kuwatumikia Watanzania. Ni kwa bahati mbaya sana kwako kuwa hata kama haukupenda itokee lakini Mungu alipenda iwe ilivyo sasa. Kwa hili umefeli. Jipange na Timu yako, tukutane 2025.