Dkt. Bashiru ni Sauli aliyegeuka Mtakatifu Paulo

Dkt. Bashiru ni Sauli aliyegeuka Mtakatifu Paulo

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935
Je, Majambazi wakivamia eneo ulipo wewe, na kisha wakati uvamizi ukiendelea akatokea Jambazi mmoja akujuaye binafsi, ambae kumbe ni jirani yako kule mtaani kwako.

Ila kwa bahati mbaya mmekutana akiwa kazini ila asiyetaka wewe jirani yake udhurike au kuuawa!

Tena Bila hata kujali kwamba kupona kwako,ni hatari kwake na majambazi wenzie huko mbeleni dhidi ya kuwataja kwa Polisi.

Na akakupigia kelele ulale chini ili kuepa Risasi ya Jambazi mwenzake aliyeko nyuma yako,aliyekulenga kutaka kukupiga Risasi wewe!

Utaacha kutii tahadhari ile kutoka kwa jirani yako jambazi ili kujiokoa na kutulia ukisimama wima ili Risasi ikupate bila kulala chini?

Eti Kisa tu anayekutahadharisha ni Jambazi mwenzao?

La hasha! Tahadhari imetoka Moyoni kwa mtoa tahadhari. Haitoki mdomoni bali imepitia hapo mdomoni ili kumfikia mtahadharishwa!

Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.

Pia hata wasio na nguvu au mamlaka,lakini wanao uwezo wa kuyaona na kuyajadili yanayokuwa yakitendwa na wanasiasa walioko kwenye siasa za moja kwa moja kiutendaji.

Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi.

Hivyo basi huwezi ukamzuia Bashiru kuyasema yale ambayo ametasema, kulingana na upeo wake yeye kwa wakati husika, tofauti na upeo aliokuwa nao wakati ule.

Huwezi iharamisha tahadhari sahihi kwa wannchi, eti kwa sababu imetoka kwenye kinywa kisicho Sahihi?

Pia watu wengi walikuwa wakimsifia Magufuli (R.I.P), sio kwa ukatili wake,bali walimsifia kwa utendaji na mtindo wake wa Utoaji Maamuzi.

Ambao kutokana na hali ya wakati husika ilivyokuwa imefikia,alionekana kama Muarobaini wa magonjwa ya wakati ule! Ambayo tayari yalikuwa Sugu.

Na huko tuendako sasa,ni kama vile atahitajika Magufuli mwingine tena,ili kuyatibu yale tunayougua kwa sasa!JUA JINSI YA kutumia milele na Mungu. Pata msamaha kutoka kwa Mungu

SWALI
Je, tunaweza kujifunza nini kutokana na maisha ya Paulo? Paulo alikuwa nani?

JIBU
Kuna mengi tunaweza kujifunza kutokana na maisha ya mtume Paulo. Mbali na kawaida, Paulo alipewa fursa ya kufanya mambo ya ajabu kwa ufalme wa Mungu.

Hadithi ya Paulo ni hadithi ya ukombozi katika Yesu Kristo na ushahidi kwamba hakuna mtu aliye zaidi ya neema ya kuokoa ya Bwana.

Hata hivyo, ili tupate kipimo kamili cha mwanadamu, ni lazima tuchunguze upande wake wa giza na kile alichoashiria kabla ya kuwa "Mtume wa Neema." Maisha ya kwanza ya Paulo yaliashiria raghba ya kidini, ukatili wa nguvu, na mateso yasiyo na huruma ya kanisa la kwanza.

Kwa bahati nzuri, miaka ya baadaye ya maisha ya Paulo yanaonyesha ishara tofauti kama aliishi maisha yake kwa ajili ya Kristo na kwa maendeleo ya ufalme Wake.

Hivyo tusimbeze Dkt Bashiru,bali tuyatumie Maneno yake kama yatakuwa yanatufaa.

Alamsikhi.
10101.
 
Machawa wote wa Magufuli wasulubiwe.

Ni Heri timu ya majiziya msoga kuliko hawa wasaliti wauwaji wa demokrasia.
 
Machawa wote wa Magufuli wasulubiwe.

Ni Heri timu ya majiziya msoga kuliko hawa wasaliti wauwaji wa demokrasia.
Kweli kwa sababu Msoga anaishi na wezi,lakini Magufuli alkamata na kuwasulubu wezi!

Kwa sababu Msoga anaishi na vyeti fake lakini Magufuli aliwatimua na kuwarudisha makwao.

Ni kweli Msoga waliishi wabadhiilifu,lakini Magufuli aliabana na kuwatemesha kilichoibwa nao!

Ndio maana China watu sampuli ya Msoga wanakula za kifuani Chap!

Kama unabisha muulize Mjukuu wa Msoga na kijana wa kaa- Kwata akusimulie yaliyomsibu ipojaribu huo ujinga kule China!
 
... the point is, Bashiru ana hoja au hana hoja? Kama ni hoja ya kipumbavu abaki na upumbavu wake; kama ni hoja yenye mashiko ifanyiwe kazi.

Mara nyingine hata Shetani pamoja na uongo wake wote (maana ndiye baba/mama wa uongo) hata kama ni mara chache humtoka yaliyo ya kweli. Haikupata kuwandikwa, "Nao wakaanza kupiga kelele, 'Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?'”. Tuyapinge hayo simply kwa sababu yamenenwa na ambaye uongo ndio jadi yake?

Tusimtazame aliyetoa hoja; tuijadili hoja.
 
Back
Top Bottom