Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko ameahidi kutoa kiasi cha Tsh. Milioni 10 kwenye harambee ya Ukarabati wa jengo la kanisa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Kome iliyoandaliwa na Muhashamu Askofu Flaviani Katindi Kasala wa Jimbo Katoliki la Geita, kwa kushirikiana na Baba Paroko Padri Japheth Masalu wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Kome.
Mhe.Dkt. Biteko ametoa ahadi hiyo kupitia mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda.