ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Dkt. Kimei amesema kuwa kwa sasa benki zinapata faida kubwa sana, jambo ambalo anaona kuna tozo au gharama ambazo benki hazifichui kwa wazi kwa wateja.
Ametolea mfano kuwa benki zimejipatia faida ya Trilioni 1.6, lakini ukuaji wa uchumi hauakisi faida hiyo. Amesema ni wakati sasa kwa watendaji wa benki kuhakikisha kuwa wawekezaji na wateja wanapata manufaa kutokana na huduma za kibenki badala ya kuwanyonya.
Dkt. Kimei amesisitiza kuwa mwenendo huu wa kuwanyonya wateja hauonyeshi ishara nzuri kwa benki. Anahimiza benki zitilie maanani maslahi ya wateja na kuchangia katika maendeleo ya uchumi kwa njia endelevu.