TAMU YA LEO
Member
- Mar 26, 2020
- 8
- 3
Mwandishi Wetu
Vunjo
Kukosekana kwa elimu shirikishi juu ya wadau wa sekta za kifedha katika jimbo la Vunjo kumepelekea wananchi walio wengi kushindwa kunufail na mikopo hususan inayotolewa na serikali.
Dkt. Charles Kimei ambaye ni mgombea ubunge jimbo la Vunjo (CCM)alisema kazi mojawapo iliyopo mbele yake nikuona namna ya kutoa elimu kwa makundi ya vijana na akina mama ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Alisema zipo taasisi mbalimbali za kifedha pamoja na serikali lakini walengwa haswa au wanufaika hawana uelewa wakutosha katika sekta hiyo.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara kata ya Kirua Vunjo kusini eneo la Uchira alisema kipaumbele ni kuhakikisha wananchi wa Vunjo wananufaika na fursa za kiuchumi pindi zinapojitokeza.
''Kuna mfuko wa Rais,zipo fedha kwa akina mama na vijana na pia wapo wadau mbalimbali wakimaendeleo ni lazima nikaunganishe kwa pamoja ili wanavunjo waweze kunufaika''alisema
Kuhusu masoko nikuwayakiboreshwa yataweza kuvutia watalii kufanya manunuzi katika eneo la Vunjo tofauti na ilivyo sasa kuwa wanaenda jijini Arusha na maeneo mengine hivyo kufanya mzunguko wa fedha kuwa chini.
''Ukiwa na masoko ambayo ni mazuri ni dhahiri kuwa kutakuwa na muingiliano wa watu wengi na hapo ndipo ubunifu wa kibiashara unapoanzia na kuanza kukua kwa kipato''alisema
Dk Kimei alisema baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba ni lazima atumie elimu yake katika utaalamu wa fedha kuviwezesha vikundi vya vijana,walemavu,na akina mama namna yakuchangamkia fursa za mikopo.
Alisema serikali ya awamu ya tano imetilia mkazo kwa kila halmashauri kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mkopo usiokuwa na riba lakini ni watu wachache sana wenye uelewa katika hilo.
Samwel Shao ni mgombea udiwani kata ya Mwika Kaskazini (CCM)ambapo alisema baada ya kuchaguliwa ni lazima aanze na vikundi vya vijana na wanawake ili ahakikishe nao wanafaidi keki ya taifa kama ilivyo kwa maeneo mengine.
Alisema fursa za kujikwamua kiuchumi zipo ila tatizo ni kukosa uwakilishi sahihi wenye kuwa na maono na nia njema ya mafanikio badala yake ni uwepo wa wawakilishi wenye ubinafsi.
Mwisho.