Dkt. Damas Ndumbaro: Fanyeni Sanaa Kibiashara

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ametoa wito kwa wadau wa sekta ya Utamaduni na Sanaa nchini wafanye kazi hiyo kibiashara ili wanufaike zaidi.

Dkt. Ndumbaro amesema hayo Oktoba 12, 2023 jijini Dar es Salaam alipotembelea Ofisi za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa nchini.

Akiwa katika ziara hiyo, amemuagiza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Bi. Nyakaho Mahemba ahakikishe kuwa anashirikiana na Benki ambazo zinatoa mikopo hiyo kutoa mafunzo kwa wadau hao kabla ya kuwapatia fedha ili lengo la Mfuko huo litimie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…