Dkt Doroth Gwajima, tafadhali tufafanulie kama fedha za TASAF: Ni Mali ya chama au Serikali?

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Dkt Doroth Gwajima ni Kipenzi cha watu wa mitandaoni maana anajibu kistaarabu na anachukua hatua Kwa Malalamiko anayoyapata mitandaoni.

Aje atufafanulie kama madai ya hawa Wananchi wa Kasulu ni kweli au uzushi? Kama ni kweli, sharti la kuwa na kazi ya chama liko kwenye Sera ya uchumi au sheria ya Mfuko wa TASAF?

"Fedha tunayopokea kupitia mfuko TASAF ni pesa kidogo lakini kinachotuuma zaidi ni kwamba ili tupokee mgao huo tunalazimishwa kuwa na KADI YA CCM. Nilipohoji kuwa ni mradi wa CCM au serikali au unatoka wapi niliondolewa kwenye mfumo wa kupokea gawio hilo."

Soma Pia: Wanufaika wa TASAF washauriwa kubuni vyanzo vya mapato ili wapate maendeleo na kutoka kwenye umaskini

Wananchi
📍Kasulu DC

Tafadhali Wananchi tunaomba jibu.

67.jpg
 
hatari sana
hii nchi viongozi wanatufanya wananchi ma zwazwa
 
Una uhakika gani kuwa huyo mama hajalishwa MANENO na maadui wa CCM ?!!

Tutindaga mbona unahukumu haraka hivi?!? [emoji44][emoji44]
Kijana haya mambo tunayotenda kuna siku yataturudia. Tusifanye siasa kama Simba na Yanga. This is serious, niggas are starving out there. Sijajua unafaidika na nini kwa haya unayohubiri hapa jukwaani. Ila siku tembelea vijiji angalia maisha wanayoishi, kula wanachokula, kunywa maji wanayokunywa. Halafu rudi hapa andika tena hisia zako.

Sijui unajifungia chumbani au vipi, ila kwa sasa maadui wa CCM kama unavyowaita sio CHADEMA tena, wala CUF wala ACT. Ni Wananchi wenyewe. Angalia wanavyokua negative kwa kila jambo serikali inalofanya, bahati mbaya wakati mwingine serikali inafanya jambo jema na bado wana Crash.

Hii sio dalili nzuri kwa Serikali, Sio dalili nzuri kwa CCM.

Nakukumbusha tu, mtu anapopata ujasiri kuibua jambo ambalo litanufaisha jamii nzima na wewe ambaye una uhakika wa shibe yako ukaja kuingiza siasa kuna siku yako itafika.

Kanuni ni ile ile, Kiendacho kikizunguka, Hurudi kikizunguka. Hili sio onyo, Hii ni taarifa.
 
Ok mkuu nimekusikia.....

Ila hoja ni moja tu....tunazungumzia kilichowekwa humu ndani....kipindi hiki cha kukaribia chaguzi...una uhakika na ushahidi gani kilichosemwa kikakusukuma UTOE HUKUMU....

Haiwezekani hili ni PICHA la kadenge linalotumiwa na wanasiasa kinzani ?!!!
 
Back
Top Bottom