Dkt. Dorothy Gwajima akemea tabia ya baadhi ya wanawake kujitangaza ukahaba mtandaoni Mitandaoni

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Siku hizi baadhi ya wanawake wamekuwa wakiitumia mitandao ya kijamii kujitangazia biashara ya ukahaba wanayoifanya jambo linalohatarisha usalama wa maadili katika jamii yetu.

KUpitia mtandao wake Instagram Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima amekemea vikali wanawake wanaojidhalilisha kwa kufanya mambo yasiyofaa mitandaoni badala yake amewataka wanawake wote nchini kutumia fursa halali za maendeleo ya jamii ili kujipatia kipato halali.


=========
Sasa,

1. Wahusika wa video hii na tangazo hilo, mna leseni ya biashara hii mnayotangaza? Maana huwa hakuna leseni ya mambo haya yaliyo kinyume na maadili, hivyo hakuna uhalali wa Tangazo hili.

2. Nyie mabinti mnaojitangaza, ni sehemu ya wanawake ambao kila siku tunalia tunanyanyaswa tunahitaji kuheshimiwa kwa sheria kali kali: itawezekanaje wakati sisi ndiyo tuna promote mkao wa kukatiliwa?

3. Kama ni biashara halali, mbona inawezakana kupitia mikopo ya wanawake tunayotangaza kila siku. Shida ni hatujui au uvivu na kutaka hela za haraka haraka?

WITO; Kwanza msitishe hili jambo ambalo awali ni kinyume na Sheria zote, kisha nakuja huko mje mniambie shida nini hadi mnafikia hali hii kwenye nyakati hizi zenye fursa za kutosha kufanya biashara halali.......

Katika kuja kwangu huko, nawasiliana na MKUU WENU WA WILAYA kwanza.....

TUACHE KUJIDHALILISHA WENYEWE na kufungua milango ya kudhalilishwa na wengine. TUTUMIE FURSA HALALI ZA MAENDELEO YA JAMII.

"hii picha ni kutoka kipande cha video kinachosikika kikitangaza biashara niseme ya ukahaba huko kunakoitwa 'LIQUID BAR'. Video hii WENGI MNAIJUA maana IMEZUNGUKA SANA na nimetumiwa mara kadhaa"
 
Waanze na Bongo movies + wasanii wa music hawa ndio chanzo kikubwa cha haya yote, hawa woote unaowaona ni baada ya kuwaona akina Wolper, Uwoya, Gigi nk kama role models wao.

Kama tumeamua kusimamia maadili basi tuwe serious hata kwa yale yanayotufurahisha na kutuletea wapiga kura.
Kuna hawa waenda harusini wanafanya mambo ya ajabu mabarabarani, na huko uswahilini vigodoro visivyo na mipaka, kwenye kampeni zetu za siasa, sherehe za mwenge nk.
 
2. Nyie mabinti mnaojitangaza, ni sehemu ya wanawake ambao kila siku tunalia tunanyanyaswa tunahitaji kuheshimiwa kwa sheria kali kali: itawezekanaje wakati sisi ndiyo tuna promote mkao wa kukatiliwa?


Usipo jithamini utathaminiwa na nani? Mr Ebbo
 
Kutokea hapa magomeni mapipa nafikaje hapo liquid bar nikawakemee hao warembo, hivi vitendo sisi wanaume tuwe mstari wa mbele kukemea.
 
Kutwa kuonesha makalio yao makubwa na kuyatikisa huko mtandaoni

Ova
 
2. Nyie mabinti mnaojitangaza, ni sehemu ya wanawake ambao kila siku tunalia tunanyanyaswa tunahitaji kuheshimiwa kwa sheria kali kali: itawezekanaje wakati sisi ndiyo tuna promote mkao wa kukatiliwa?


Usipo jithamini utathaminiwa na nani? Mr Ebbo
'Usipo jithamini utathaminiwa na nani? Mr Ebbo'📌📌Na bado wanadai haki sawa...
 
Huyo Gwajima ameshawahi kuwafuata akawauliza kwanini wanajiuza. Maana sio haba mtu azaliwe Alfu aamue tu kujiuza lazima kuwe na kitu kilichompelekea kufanya hivyo

Afya ya akili ni muhimu tusiwa judge watu hatujuwi walichopitia ma kuamua kuchukua maamuzi hayo
 
Pisi zenyewe zimechoka balaa!
 
Umasikini + mfumo mbovu wa elimu kuanzia msingi mpaka chuo kikuu + Feminism + Beijing Conference

Wahanga wakubwa wa hayo yote ni wanawake ambao hawana uwezo wa kupambana na mikikimikiki ya dunia na ukizingatia wanaume sasa wameamua kumfanya mwanamke chombo cha starehe na sio mshirika wa kutengeneza familia.

Wanawake kujifanya wanahaki sawa kama wanaume kumelifanya kundi kubwa la akina mama kuachwa mitaani bila msaada maana nao wanauwezo wa kutafuta hela matokeo wamebaki kwenye kazi rahisi rahisi ambazo hazilipi, zinahitaji elimu na ni chache, kule kwenye mikiki ambapo ndio kunalipa, kunahitaji watu wengi nk ni kugumu kwao kutokana na maumbile Yao matokeo yake wanajikuta hawana option tena maana ile huruma ya zamani ya mwanaume haipo baada ya mwanaume kumuona Mwanamke kama mshindani mwenzie.

Jamii irudi kwenye drawing board iangalie upya mustakababli wa Mwanamke ikiwa ni pamoja na kuwarudisha kwenye uhalisia wao wa umama, watunza familia na washiriki wa familia bora na sio washindani wa mwanaume.

Hatuwezi kupambana na Asili.
 
yeye anakula hela ya uma wenziwe wanani? kama ni rahisi angevaa viatu vyao. Aache kiherehere
 
Yaani ni aibu tupu ,ukiingia facebook na insta yaani ni maskin tyt yanayoonyesha maungo na makalio tu ,sijui wamepatwa na nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…