Dkt. Doto Biteko: Usichukue muda mwingi kulinda cheo, chukua muda mwingi kutoa matokeo katika kazi yako

Dkt. Doto Biteko: Usichukue muda mwingi kulinda cheo, chukua muda mwingi kutoa matokeo katika kazi yako

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka Watumishi wa Wizara yake kutumia muda mwingi kufanya kazi na sio kulinda vyeo vyao.

Waziri huyo amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake jijini Dodoma.

“Usichukue muda mwingi kulinda cheo, chukua muda mwingi kutoa matokeo katika kazi yako, cheo hakilindwi. Kama kilivyokuja bila wewe kukipambania kitaondoka siku moja utake au usitake na atakuja mtu mwingine kwa sababu na wewe ulikuta mtu mwingine,” amesema Dkt. Biteko.

PIA SOMA
- Dkt. Biteko azitaka Mamlaka za Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki kuzingatia weledi, maadili na uwajibikaji

 
Ila viongozi wa ccm bhana. .Wanachokitamka mdomoni ni tofauti na kilichopo moyoni.
 
Zilongwa mbali zitendwa mbali.

CCM mbona wanafanya hayohayo sasa.
 
Back
Top Bottom