Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Dkt. Biteko amesema hayo leo May 31,2024 wakati wa uzinduzi wa kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Ifakara.
Biteko amesema “Mahitaji ya umeme kwenye Nchi yetu sio anasa ni jambo la lazima kwasababu Wananchi wanao uhusiano wa moja kwa moja wa maendeleo yao na nishati ya umeme, hatuna sababu yoyote ya kuja kwa Wananchi kuwaambia mipango bila kuona matokeo, Wananchi wangetamani kuona mipango inayotafsiriwa kwa thamani ya fedha lakini muhimu zaidi kwa mipango ambayo inatekelezeka”
“Kituo hiki maana yake ni kwamba mwaka jana wastani wa masaa ya umeme kukatika kwenye eneo hili ilikuwa ni masaa manane kwa mwezi, maana yake ukichukua dakika ambazo umeme umekatika utakuta hakuna mgao lakini umekatika ni masaa manane, ninafurahi kusema kwa mwezi huu ambao tunaumaliza matukio ya kukatika umeme ni dk 49 pekee yake kutoka masaa manane na hata hizi dk 49 ni kwenye laini ambazo tulikuwa na matengenezo ya kinga ambazo Wateja walipewa taarifa”