Pre GE2025 Dkt. Emmanuel Nchimbi: Kulikuwa na majambazi CCM wanaotoa rushwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema chama hicho kimefanya mabadiliko ya kuongeza wajumbe katika Mikutano Mikuu ya Kata na Mikutano Mikuu ya Wilaya ili kupunguza mianya ya rushwa iliyokuwa ikifanywa na watia nia ili kupitishwa na chama kugombea udiwani na ubunge.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Dkt. Nchimbi ameyabainisha hayo Februari 19 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa kata na makatibu tawi wa mkoa wa Dodoma na kueleza kuwa kulikuwa na tabia ya watia nia kutoa fedha(rushwa) kwa wajumbe wa mikutano mikuu ili wawapitishe kitendo ambacho amekiita ujambazi kwani wahusika walikuwa wakishachaguliwa hawafanyi kazi wanasubiri tena uchaguzi ufike watoe rushwa na kupitishwa.

Yeye mbona alipewa pesa kipindi kile cha team lowasa ili akae kimya na wana mtandao wenzake.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema chama hicho kimefanya mabadiliko ya kuongeza wajumbe katika Mikutano Mikuu ya Kata na Mikutano Mikuu ya Wilaya ili kupunguza mianya ya rushwa iliyokuwa ikifanywa na watia nia ili kupitishwa na chama kugombea udiwani na ubunge.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Dkt. Nchimbi ameyabainisha hayo Februari 19 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa kata na makatibu tawi wa mkoa wa Dodoma na kueleza kuwa kulikuwa na tabia ya watia nia kutoa fedha(rushwa) kwa wajumbe wa mikutano mikuu ili wawapitishe kitendo ambacho amekiita ujambazi kwani wahusika walikuwa wakishachaguliwa hawafanyi kazi wanasubiri tena uchaguzi ufike watoe rushwa na kupitishwa.

Yes, Mze Makamba was one of them
 
Hili kweli linaweza kwisha?
Ana bidii Nchimbi, akaze buti tu
 
Toa boriti machoni kwako kabla ya mwenzio!
Nyani kum cheka kund*le!
Chukuwachakomapema ni wababaishaji mpaka wanakuwa comedians waliobobea!
 
Back
Top Bottom