Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema chama hicho kimefanya mabadiliko ya kuongeza wajumbe katika Mikutano Mikuu ya Kata na Mikutano Mikuu ya Wilaya ili kupunguza mianya ya rushwa iliyokuwa ikifanywa na watia nia ili kupitishwa na chama kugombea udiwani na ubunge.
Dkt. Nchimbi ameyabainisha hayo Februari 19 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa kata na makatibu tawi wa mkoa wa Dodoma na kueleza kuwa kulikuwa na tabia ya watia nia kutoa fedha(rushwa) kwa wajumbe wa mikutano mikuu ili wawapitishe kitendo ambacho amekiita ujambazi kwani wahusika walikuwa wakishachaguliwa hawafanyi kazi wanasubiri tena uchaguzi ufike watoe rushwa na kupitishwa.