TANZIA Dkt. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni afariki Dunia

Nimeumizwa sana ssna
Conspiracy haikwepeki hapa.

Hakuwa mtu wa kuugua mara kwa mara. Lakini siri ya kifo ajuae Mungu

Poleni sana JamiiForums Wote kwa msiba huu mzito.
Pole nyingi kwa familia kwa kupoteza baba, mume, ndugu na jamaa
Pole nyingi kwa Mhe. Samia kwa kupoteza jembe muhimu sana.

Nanusa hujuma
 
Ni ushauri mzuri. Lakini nani atamkataza nani asiende wapi kutafuta matibabu ya afya yake mwenyewe?
Kweli hapa Kuna changamoto, lakini in the context ya government intervention ktk matibabu ya viongozi wa kiserikali, India and some countries not the right choice kwa sasa. Ni haki ya mgonjwa kwa kuzingatia uwezo wake atibiwe anapotaka lkn kwa viongozi wa kiserikali ni vizuri kuwa na right and safe country choice lkn pia kipao mbele kikiwa kuwapatia matibabu ndani ya nchi.
 
Hapo JKCI/MNH ina maana wanacheza cheza tu, maana wakubwa wote wanaenda India na kurudi kama cargo.
 
Apumzike anapostahili. Kamaliza mwendo wake sisi sote kwake tutarejea
 
Nimekuja mbio mbio nikidhani ni Faustine Mafwele, dah! Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amen
 
Ukweli ninachojua huwa ana ugonjwa wa moyo ila sikujua ni serious kiasi hiki. Hata akiwa waziri safari za kwenda check up India zilikuwa nyingi tu.
Da, kumbe alikuwa na tatizo la moyo? Hata mimi siamini kuwa kuna mchezo wowote mchafu kwani hakua tishio kwa mtu yeyote kisiasa. Anyway, nadhani kati ya CCM wachache wazuri huyu alikuwa miongoni.
 
Unajua mtu akishaugua, mara nyingi maazimio mengine yote huwa yanarukwa? Yule atakayepinga matibabu ya nje ndiye ataonekana mchawi haswa.

Halafu, suala la kuwatibia nje siyo kwamba linatokana na utaalamu zaidi. Nadhani wengi wanakimbilia huko kiusalama. Ni kama vile humu ndani hatuaminiani.

Hapo kiongozi anaona bora akazungukwe na jopo la madaktari wasiomfahamu, kuliko hawa wetu ambao anadhani wanaweza kumleftisha muda wowote hata kama siku zake hazijatimu.
 
Hapo JKCI ina maana wanacheza cheza tu, maana wakubwa wote wanaenda India na kurudi kwa kama cargo.
Hii inasikitisha sana, idara zote za kitabibu katika hospital zetu za kitaifa zimeimarishwa sana, JKCI, MNH, Mloganzila, Benjamin Mkapa Dom etc, Kwa nini viongozi wakatibiwe nje na mara nyingi wakirudi kama cargo?? Kwa hiyo wananchi wanatuhadaa wanapotuambia huduma za kitabibu ktk hosptali zetu zimaimarika kiasi cha wageni kutoka mataifa ya nje kuja kutibiwa hapa nchini?!! Kama viongozi hawawi mfano wa kuigwa tutaendelea kuwaamini vipi?!! Je, ni JPM pekee ndo alikuwa mzalendo wa kweli!
 
Mkuu, ulishawahi kutaka ukatibiwe India au SA, mtu akakuzuia kwani? Suala la kiafya - nani na wapi mtu atibiwe - ni uamuzi binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…