Dkt. Faustine Ndugulile: Mafundi simu wenye tabia ya kufuta namba ya IMEI kuchukuliwa hatua

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Serikali imesema kuwa itawachukulia hatua kali mafundi simu wote wenye tabia za kufuta namba ya kipekee inayotambulisha simu husika (IMEI) wanapopelekewa simu na wateja wao kwa ajili ya matengenezo.

MAFUNDI.jpg

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile, mkoani Arusha wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa mkoani humo alipotembelea taasisi za wizara hiyo na kutumia nafasi hiyo kuwaasa wote wenye tabia hizo kwani ni kinyume cha sheria.

Amesema kuwa baadhi ya mafundi simu wasio waaminifu wanatumika kufuta IMEI (International Mobile Equipment Identity) namba za simu za mkononi za wateja wao ili simu hizo ziweze kutumika tena ambacho ni kosa kisheria na serikali itawachukulia hatua kali mafundi watakaobainika kufanya tabia hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa TCRA Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Imelda Salum, ametoa rai kwa wawekezaji wa sekta ndogo ya utangazaji kujenga studio za redio kwenye kanda hiyo kwa kuwa baadhi ya maeneo hayana usikivu kwani kwa kufanya hivyo kutachochea maendeleo ya wananchi kwa kuwa kanda hiyo ina fursa katika sekta ya utalii na hivyo vifaa na huduma za mawasiliano vinatumika ipasavyo.
 
Mimi pia ningependa ufafanuzi amaanisha ni ?

Je, mafundi wasinunue simu za wizi na kuzibadilisha identity?
 
Huyu nae hachoki ?! Hajamaliza hili kasharukia hili.
 
Serikali imesema kuwa itawachukulia hatua kali mafundi simu wote wenye tabia za kufuta namba ya kipekee inayotambulisha simu husika (IMEI) wanapopelekewa simu na wateja wao kwa ajili ya matengenezo.

MAFUNDI.jpg

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile, mkoani Arusha wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa mkoani humo alipotembelea taasisi za wizara hiyo na kutumia nafasi hiyo kuwaasa wote wenye tabia hizo kwani ni kinyume cha sheria.

Amesema kuwa baadhi ya mafundi simu wasio waaminifu wanatumika kufuta IMEI (International Mobile Equipment Identity) namba za simu za mkononi za wateja wao ili simu hizo ziweze kutumika tena ambacho ni kosa kisheria na serikali itawachukulia hatua kali mafundi watakaobainika kufanya tabia hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa TCRA Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Imelda Salum, ametoa rai kwa wawekezaji wa sekta ndogo ya utangazaji kujenga studio za redio kwenye kanda hiyo kwa kuwa baadhi ya maeneo hayana usikivu kwani kwa kufanya hivyo kutachochea maendeleo ya wananchi kwa kuwa kanda hiyo ina fursa katika sekta ya utalii na hivyo vifaa na huduma za mawasiliano vinatumika ipasavyo.
Mazungumzo baada ya habari
 
Back
Top Bottom