Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amejumuika na wananchi wa Wilaya ya Siha katika kata za Mung’e na Miti Mirefu kwa shughuli za uchimbaji mitaro kwa ajili ya kusimika mabomba ya maji. Sambamba na hilo, amezindua mradi wa maji katika kata ya Miti Mirefu, mradi ambao unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 3,600.
Shughuli hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji, ambapo serikali imeendelea kuhamasisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi. Dkt. Mollel aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo ili kuhakikisha huduma za msingi zinaimarika katika jamii zao.