Prof Janabi anakitu, ila wachache labda kwa kutokujua wanaweza wasimwelewe. Wengi watu maaeufu kwenye mitandao hawajiineshilakini inawezekana hata majumbani mwao wanawataalam wa Tiba lishe/asilia kwani ndio asili ya mwanadamu na Tiba yake haiachi chemicali za simu mwilini.
Hapa Mh Raisi anastahili pongezi kwa kuliona hili.
Ikiwezekana kianzishwe/vianzishwe vituo vya Tiba lishe/ asilia vya serikali kabisa ambayo vitatoa Tiba hio (Ikiwezekana kwa Kambi hadi waponapo) , kwani wengi huishindwa kwasababu ya ugumu wa maandalizi ya Tiba hizo.
Tutakubaliana hapo zamani ilikuwa akionekana mtu anatembeza unga wa mbegu za komamanga, au mlonge, au mbegu za parachichi ilikuwa ningumu kueleweka. Tujiulize kwanini hivi Leo Tiba hizi hukubalika kwa Kasi? Jibu ni rahisi kuwa watu wengi wameshaona matokea kwa lishe hizi asilia.
Kibaya nikuwa kunawimbi limeingia kwa kigezo Cha kibiashara, wakulima wanahamasishwa kungoa miti ya matunda asilia na kupanda mimea isiyo asili GMOs.
Je tuthamini fedha kuliko afya na uhai wetu? Fedha zitamsaidia nani? Tunamikakati gani ya kuilinda mimea yetu asilia pale tunapoikata/ng'oa na kupanda mimea ya kisasa?
Shida ya magonjwa yasiyoambikizwa kama cancer zaidi ni kwa nchi za vipato vya kati na chini (70%) . Labda nikwasababu ya mfumo duni wa ulaji(zaidi wanga) hapa ni wali, ugali, akijitahidi chips, migogo.
Miili inatengeneza sumu, seli za mwili zinabadilka kutoka uhalisia wake matokeo ni cancer, kisukari,magonjwa ya moyo.
Tiba lishe hizi zikikubaliwa na kutiliwa maanani ni Imani kuwa idadi ya wagonjwa ocean road nakwingineko itapungua.