Papaa Muu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 243
- 292
Na; Makame Ali Makame
11/10/2020
Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi amebainisha mara kadhaa dhamira yake ya kulinda na kuheshimu Katiba yetu kama Mkataba maalum baina yake na wananchi wote. Ukifuatilia kwa makini kampeni za Dr. Hussein Mwinyi utabaini kwamba yeye ni mgombea mwenye staili ya pekee katika kunadi vipaumbele vyake. Dr. Mwinyi ameamua kuachana na mambo ambayo yalikwisha kufanyiwa kazi na amejikita kuendelea na juhudi za kuimarisha maisha ya watu kwa kuendeleza pale walipoishia viongozi wenzake au kuibua masuala muhimu yatakayoinufaisha Zanzibar na Tanzania.
Maridhiano ya Wazanzibari ni suala la Kikatiba, limo ndani ya Katiba na lina taratibu zake maalum. Kwa kuwa ahadi ya Dr. Mwinyi ni kulinda Katiba, ni wazi kwamba Maridhiano ya wazanzibari ni katika masuala atakayoyapa umuhimu wa hali ya juu kwani mara kadhaa ameonesha waziwazi kuumwa kwake na mgawanyiko wa wananchi unaosababishwa na mambo kadha wa kadha na kupaliliwa na watu walioishiwa.
Serikali ya CCM iliridhia, ilianzisha na ilisimamia Maridhiano ya Wazanzibari yaliyopelekea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa (GNU). Kama ilivyokuwa nia njema ya Viongozi wa CCM waliopita, Dr. Hussein Mwinyi amedhihirisha mara kadhaa nia, dhamira na malengo yake kwa Umoja wa Kitaifa na masikilizano miongoni mwa Wazanzibari.
CCM inaamini kwa dhati umuhimu wa Umoja wa Kitaifa miongoni mwa Wazanzibari ndio maana viongozi wake walichukua kila juhudi kuyastawisha Maridhiano hayo. Hata pale upinzani waliposusia Uchaguzi, wapinzani wengine walijumuishwa katika Serikali ya CCM kwa dhamira ile ile ya kuwaunganisha wazanzibari na kujumuisha mawazo mbadala katika uendeshaji wa nchi. Hata pale CCM ilipokuwa na idadi kubwa ya wingi wa kura na nguvu ya maamuzi katika Baraza la Wawakilishi hawakufuta Ibara hata moja ndani ya Katiba inayozungumzia Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Haya tunayoyashuhudia sasa ya wapinzani kushikilia ajenda ya Maridhiano na kumtaka mgombea wa CCM kusema kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU)ndio pumzi yao ya mwisho. Viongozi wa upinzani wa ACT wamejikita kuzungumzia ajenda hii kwa lengo la kuwashawishi wazanzibari ili waaminiwe kwamba bila ya wao kamwe Zanzibar haiwezi kuendelea na katu kama si wao hatua ya Maridhiano ya Wazanzibari yaliyofikiwa chini ya Seriklai ya CCM yasingepatikana.
Pamoja na mbinu hiyo, Viongozi wa ACT wanatumia hoja ya Maridhiano kuzima moto wa maswali magumu yanayoulizwa na wananchi waliobaini mbinu za viongozi hao kuvuruga Maridhiano ya wazanzibari kwa kule kususa kwao kushiriki Uchaguzi wa Marudio na ahadi zao kemkem ambazo zimeishia patupu. Msisitizo wao kuhusu ajenda ya Umoja wa Kitaifa ni kujitafutia njia ya kujipatia nafasi ya kuwemo katika Serikali ili kuwapa uhalali wa kisiasa ili kukinufaisha kikundi chao cha watu wachache.
Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi pekee ndiye mwarubaini ambao utaondoa mgawanyiko wa wananchi Visiwani Zanzibar ulichochewa na viongozi wa vyama vya upinzani walioishiwa kisiasa.