Dkt. Jabir Bakari: Asilimia 27 pekee ya Watanzania ndio wanamiliki Simu janja (Smartphone)

Dkt. Jabir Bakari: Asilimia 27 pekee ya Watanzania ndio wanamiliki Simu janja (Smartphone)

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Bakari amesema hadi takwimu za mwezi January mwaka huu ni Asilimia 27 pekee ya Watanzania ndio wanamiliki Simu janja (Smartphone) na kusema malengo ya Serikali ni kuhakikisha Watumiaji wa Smartphone wanafikia 100%,

Dr. Jabir amesema kwamba gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine zimeshuka kutoka Tsh. 2. 6 kwa dakika mwaka 2021 hadi kufikia Tsh. 2.0 kwa dakika kwa mwaka 2022.

Dr. Jabir ametoa pia takwimu kutoka kwenye tafiti mbalimbali ambazo zinaonesha Kati ya Nchi 155 Ulimwenguni, Tanzania inashika nafasi ya 21 kwa unafuu wa gharama za kununua GB 1, pia Tanzania inashika nafasi ya 6 kwa unafuu zaidi wa gharama ya data kati ya Nchi 55 Barani Afrika.

Dkt. Jabiri ameelezea pia kwa undani kuhusu malalamiko ya wanaodai kuibiwa bando zao na amezitaja sababu zinazopelekea bando kuisha haraka....

Chanzo: Millard Ayo
 
Kwa mwendo huu wa 1gb 2000.

Watafanikiwa wakiwa wamechoka sana.
 
Na smartphone tumejaza porno aka connection na namba za michepuko kama vile "aisha msambwanda", mariamu kibindankoi" nk
 
Watafanya nini kuhakikisha hiyo 100%? Kuna mambo mengi ya kutilia mkazo kabla ya simu, upuuzi upuuzi tu.
 
Watafanya nini kuhakikisha hiyo 100%? Kuna mambo mengi ya kutilia mkazo kabla ya simu, upuuzi upuuzi tu.
kwenye hiyo 100 kuna vichaa,watoto ,walemavu mfano vipofu na masikini hivo haitowezekanA kufikia
 
Simu janja bei kubwa wapunguze kodi hiki watu wengi wazimudu zaidi pia mitandao ya simu wamejitaidi kuboresha upatikanaji wa mawasiliano ya internet japo badi bando lipo juu kwa kiasi flani

Mrusi mweusi

Sent from my Nokia 2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom