Uchaguzi 2020 Dkt. John Pombe Magufuli sio mbinafsi ndio maana amefanya makubwa kwa muda mfupi, anastahili mitano mingine

Uchaguzi 2020 Dkt. John Pombe Magufuli sio mbinafsi ndio maana amefanya makubwa kwa muda mfupi, anastahili mitano mingine

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Ili kiongozi aweze kuleta maendeleo katika taifa lake ni lazima asiwe mbinafsi. Maana kuwa na sera nzuri au ilani ya chama nzuri sio sababu ya kuleta maendeleo.

Tanzania ni nchi ambayo imepata kiongozi ambae amewashangaza watu wengi duniani na hata hapa Tanzania. Maana kwa miaka minne tu wameshuhudia maendeleo makubwa mno. Kila sekta imepata maendeleo makubwa kwa muda mfupi, sekta ya afya, elimu miundo mbinu na hata nishati ya umeme.

Miradi mikubwa inatekekezwa, mfano ni ujenzi wa SGR, JNHPP, madaraja ya Busisi na Wami, hii ni mifano tu.

Lakini nini kilichopelekea haya kufanyika? Ni kuwa na kiongozi ambae sio mbinafsi na fisadi. Maana mapato ya serikali yanatumika inavyotakiwa,kwa kudhibiti rushwa na ubadhirifu. Na kama kiongozi kama huyu angekuwa ni mbinafsi basi mapato yaliyoongezeka toka bil 800/hadi tril 1.6 kwa mwezi angeweza kujichotea na kwenda kuyaficha ughaibuni kama tunavyosikia baadhi ya viongozi wa nchi zingine za kiafrika ambazo viongizi wake wanapora mali za nchi zao na kuzipeleka Ulaya na Marekani.

Lakini sababu sio mbinafsi na sio mtu wa kutaka kujitajirisha ameona kuwa kumbe nchi yetu ina mapato mengi tu ambayo yanaweza kutumika kuwaletea wanachi maendeleo. Na ndio maana kwa muda mfupi tuneshuhudia mabadiliko makubwa mno katika kuleta maendeleo ya watu kwa kuimarisha miundo mbinu, sekta ya afya, elimu na hata upatikanaji wa nishati ya umeme. Hivyo anastahili apewe miaka mingine mitano ili afanye mengine makubwa kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom