Dkt. Kalemani: Watazania 15000 wataajiriwa katika ujenzi wa bomba la mafuta

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewataka Wananchi watakaopitiwa na ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kujitokeza na kuzitumia fursa mbalimbali ambazo zitapatikana wakati wa ujenzi wa bomba hilo

Dkt. Kalemani amesema watanzania zaidi ya 15,000 wataajiriwa katika kipindi cha ujenzi wa bomba hilo

Waziri amesema hayo akiwa Wilayani Misenyi, Kagera

 
Tozo vipi?
 
Huu ni mradi WA kisiasa. Hakuna kitakachofanyika Hadi 2025 trust me
 
Hao 15000 ni skilled au unskilled labour?
 
Km atapewa tenda mchina. Hapo hakuna hela kwasabb Mchina analipa kibarua 7,000 kwa siku.
Maisha tuliyonayo kibarua anatakiwa apewe 10,000 - 20,000
 
Watanzania wanazungumzia ajira wewe unatuletea vibarua, asubuhi una kazi mchana hauna kazi! Ajira gani hizo. Waziri hebu tueleze fursa zilizopo kwenye bomba la mafuta TAZAMA kuanzia Dar mpaka Tunduma maana wenzetu mnaongea kama ni jambo jipya uwepo wa bomba la mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…