Dkt. Kijazi awataka watumishi kuwa na ratiba ya mazoezi

Dkt. Kijazi awataka watumishi kuwa na ratiba ya mazoezi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi amewataka watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kujenga mshikamano na upendo katika maeneo yao ya kazi.

Dkt. Kijazi ametoa wito huo wakati wa bonanza la watumishi lililoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii lililofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

''Mazoezi iwe ni sehemu ya maisha yetu na pia iwe ni sehemu ya kazi zetu² amesisitiza Dkt. Kijazi.

Ameongeza kuwa, Wizara yake itajipanga kuhakikisha kila mtumishi anashiriki katika kufanya mazoezi na pia kila mtumishi anashiriki kwenye mabonanza na amewataka watumishi kuendelea kuhamasishana ili ushiriki uzidi kuongezeka katika matamasha yanayokuja.

Dkt. Kijazi amefafanua kuwa Wizara itaweka utaratibu wa kuwatambua washiriki bora wa kila mwaka wanaofanya mazoezi na wanaoshiriki kikamilifu katika matamasha kama hayo na kuwapa zawadi maalumu.

Pia, amesema kuwa, Wizara itahakikisha ushiriki wa watumishi katika matamasha hayo hauishii Dodoma bali utaendelea kwenye matamasha mengine yanayofanyika nchini, kama Kilimanjaro Marathon, Ngorongoro Marathon na Serengeti Marathon.

'' Watumishi watakaofanya vizuri tutawadhamini ili waiwakilishe Wizara kwenye Marathon hizo.''Amesema.

Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Kijazi amewapongeza washiriki wote walioweza kukimbia mbio za kilomita tano kwa kupata medali na kuwataka ambao wameshindwa wajitahidi kipindi kijacho wamalize mbio hizo.

''Ni imani yangu kuwa bonanza linalokuja wote tutamaliza mbio za kilomita tano, cha msingi tuendelee kufanya mazoezi ,tusisubiri hadi matamasha haya yafike ndo tufanye mazoezi.'' Dkt. Kijazi amesema.

Dkt. Kijazi amewashukuru Dodoma Fitness Club na Muungano Fitness Club kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kufanikisha bonanza hilo na kusema kuwa uwepo wao ni chachu kwa Wizara katika kuimarisha mabonanza.

Naye, Mwenyekiti wa Jogging Clubs Dodoma, Bw.Mugisha Mujungu ameahidi kuendelea kushirikiana na Wizara kila itakapohitaji ushirikiano katika kufanya mazoezi na kuwataka watumishi wa serikali kujiunga na Jogging Clubs ili kuimarisha afya zao.

Bonanza hilo limehudhuriwa na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na washiriki kutoka Dodoma Fitness Club na Muungano Fitness Club za Dodoma.
1612076949943.png
 
Hayo maneno ni usanii tu mtumishi anayekaa kibaha na anafanyakazi posta ataamka saa ngapi afanye mazoezi na awahi kazini huku mstari mwekundu ukimsubiri!!
 
Sidhani kama tatizo la watumishi ni mazoezi

Hivi unakunywa chai na mihogo kama prof yule kule kwenye uzi ule, sasa mazoezi ya nini?

Chakula tu anachokula ni mazoezi, nani ananenepeana kwa kula mizizi na Malala nje?

Profesa keshasema watumishi wasaidiwe nini hayo mazoezi waachieni wanyamapori
 
civil servants are scrutinizing what to digest they are less concerned with how to digest food, but those who eat to ad lib are the ones concerned with how to digest.
 
Alafu utakuta anaetoa hio counselling ana kitambi.....

Anyway mazoez ni muhimu
 
Maisha ya mbongo nazoezi tosha. Achieni hela watu wanenepe waende jim wenyewe.
 
Ye mwenyewe anapiga tizi kwanza au

Ova
 
Hayo maneno ni usanii tu mtumishi anayekaa kibaha na anafanyakazi posta ataamka saa ngapi afanye mazoezi na awahi kazini huku mstari mwekundu ukimsubiri!!
Bado tunao ujinga mwingi sana juu ya afya zetu;
Kwa hiyo unadhani katibu mkuu kuwataka watumishi wafanye mazoezi yy au taasisi inafaidika na nn?

Mazoezi ni kwa ajili ya afya personally ya muhusika sema wizara ita-benefit ikiwa tu watu watakuwa fit na kwamba ina-reduce cost za medical ikibidi jambo ambalo si benefit kubwa kama anayopata muhusika akifanya mazoezi.

Ukisema hao watafanya mazoezi saa ngap sio kweli, kama mtu yupo committed anaweza fanya mazoezi sana na akaona benefits zake. 30 min zinakutisha kwenda 5kms jogging au kuruka kamba za kutosha au any workout ambayo itakufanya uwe fit. (Just indoor or outdoor workout) kama watu wanajenga nyumba wanaweka bar humo ndani wanashindwa nn kujenga kuweka sehemu ya mazoezi (Gyms).....ni vile mwamko wa mazoezi bado hatuna tumejawa na miamko ya Bar na ulaji ovyoovyo tukiamini ndo maisha ya kifahari.

Kwa kifupi Dr. Kijazi akizungunzia mazoezi ni habari pia ya kubadili mfumo wa maisha....watu wanakula ovyoovyo sana na ndo maana rate ya vitambi (deposit) kwa wengi wetu imekuwa kubwa na matokeo watayapata immediately.

Mimi naishi Makabe nafanya kazi maeneo ya posta ya zamani, ninaamka saa 11kasoro Alfajiri nakimbia 10Kms kwa 50 hadi 60min (pace ya 5 au ya 6) kila baada ya siku 1 na nimeweza sana kupunguza ndambi na manyama zembe sina tena mafuta huu ni mwaka wa 4 nafanya hvy. Kwa mwezi min nakimbia km 120 Max 200 maana weekend nakimbia Km 21.1 hadi 42.2 km inategemea na mood. Hali hii nimeiweza na ndiyo masiha yangu ya kila siku. I take little wanga, mavyakula ya kukaanga No, beer occursionally mara 1 kwa miezi 3 tena 2 au 3 basiiii.....

Hili suala linawezekana kbs ni vile tu sisi wabongo tunaona kama mazoezi ni ubishoo which is not true.

No body is responsible kwenye afya yako except yourself.
Tubadilike mazoezi ni muhimu sana!!!
 
Huo mlo wa kukuwezesha kufanya hayo mazoezi unatoka wapi, bajeti ya chai na chakula cha mchana kwa mtumishi anaitoa wapi kwa huo mshahara duni na aendeshe familia yake..haya mambo mengine muwe mnakaa kimya tu...
 
Bado tunao ujinga mwingi sana juu ya afya zetu;
Kwa hiyo unadhani katibu mkuu kuwataka watumishi wafanye mazoezi yy au taasisi inafaidika na nn?

Mazoezi ni kwa ajili ya afya personally ya muhusika sema wizara itabenefit ikiwa tu watu watakuwa fit na kwamba inareduce cost za medical ikibidi jambo ambalo si benefit kubwa kama anayopata muhusika akifanya mazoezi.

Ukisema hao watafanya mazoezi saa ngap sio kweli, kama mtu yupo committed anaweza fanya mazoezi sana na akaona benefits zake. 30 min zinakutisha kwenda 5kms jogging au kuruka kamba za kutosha au any workout ambayo itakufanya uwe fit. (Just indoor or outdoor workout) kama watu wanajenga nyumba wanaweka bar humo ndani wanashindwa nn kujenga kuweka sehemu ya mazoezi.....ni vile mwamko wa mazoezi bado hatuna lkn ukweli ni kwamba mazoezi ni muhimu sana.

Kwa kifupi Dr. Kijazi akizungunzia mazoezi ni habari pia ya kubadili mfumo wa maisha....watu wanakula ovyoovyo sana na ndo maana rate ya vitambi (deposit) kwa wengi wetu imekuwa kubwa na matokeo watayapata immediately.

Mimi naishi Makabe nafanya kazi maeneo ya posta ya zamani, ninaamka saa 11kasoro Alfajiri nakimbia 10Kms kwa 50 hadi 60min (pace ya 5 au ya 6) kila baada ya siku 1 na nimeweza sana kupunguza ndambi na manyama zembe sina tena mafuta huu ni mwaka wa 4 nafanya hvy. Kwa mwezi min nakimbia km 120 Max 200 maana weekend nakimbia Km 21.1 hadi 42.2 km inategemea na mood. Hali hii nimeiweza na ndiyo masiha yangu ya kila siku. I tool little wanga, mavyakula ya kukaanga No, beer occursionally mara 1 kwa miezi 3 tena 2 au 3 basiiii.....

Hili suala linawezekana kbs ni vile tu sisi wabongo tunaona kama mazoezi ni ubishoo which is not true.

Tubadilike mazoezi ni muhimu sana!!!

Ume ni inspire sana mkuu kwa commitment yako na dedication ya mazoezi na fitness kwa ujumla

Nimekuelewa sababu hata mie sina excuse hata moja kwa suala la mazoezi sana labda kuna muda nakuwa tu nipo low kwenye mood ya mazoezi lkn sijawahi kuacha kwa muda mwingi na tofauti yetu labda mie muda mwingi nafanyia Gym kuanzia kuruka kamba mpaka hizo treadmills na kwa mbali nimeanza ku lift heavy kuweka ka mwili fulani

Watanzania hatuna muamko wa mazoezi na wengine huwa wakiniona wanasema kwanini nafanya mazoezi kama tu kwa muonekano naonekana nipo fit sana hawajui kwamba mazoezi ni lifestyle na ni zaidi ya muonekano kama kutokuwa na nyama uzembe mwilini ( japo hilo ni faida ya kufanya mazoezi ya mwili pamoja na afya ya akili pia unaiweka imara kwa kuwa focus na mtu chanya muda mwingi )
 
Back
Top Bottom