#COVID19 Dkt. Kimei apata chanjo, ampongeza Rais Samia

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM Mheshimiwa Dkt Charles Stephen Kimei amesema chanjo ni salama na chanjo ni kinga. Kukubali kuchanja ni kuonesha kujali afya na uhai wako pamoja na wengine.

Mimi pamoja na familia yangu tumekubali kuunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa huu hatari wa UVIKO-19 kwani zaidi ya kuathiri afya, kukatisha maisha ya wengi umeathiri sana uchumi wa mtu mmoja mmoja, Taifa na dunia kwa ujumla.

Naunga mkono na kupongeza uamuzi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuruhusu chanjo itolewe hapa nchini na kuwa hiyari kwa wananchi kuipata. Nawashauri wananchi wenzangu wa Vunjo kukubali kuchanja na kuzingatia hatua zingine za tahadhari zilizoshauriwa na wataalam wetu wa afya.

 
Mwamba anafosi uwaziri wa fedha kwa nguvu zote. Hapa ni ili bimdash amuone.
 
Angeenda na familia yake kabisa, si wamesema kuanzia 50 yrs acha wachanjwe mpaka nifike umri nitakuwa tayari nishawaona kama kuna mazombi itakuwa tayari.
 
Hyo jamaa hamna anachofanya jimbon kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…