beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei amesema Mchakato wa kulenga vikundi haufanyi kazi duniani kote akisisitiza, "Tutumie mbinu mpya kutoa mikopo hata kwa mtu mmoja mmoja. Kutoa kwa Vikundi inaleta ugumu katika uwajibikaji".
Akichangia Mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mbunge huyo ametoa wito kwa Serikali kufanyia tathmini mchakato huo, na ikiwezekana uwepo mjadala ili kuona hatua zinazoweza kuchukuliwa.