Uchaguzi 2020 Dkt. Kimei: Miundombinu ya masoko Vunjo siyo rafiki

Uchaguzi 2020 Dkt. Kimei: Miundombinu ya masoko Vunjo siyo rafiki

TAMU YA LEO

Member
Joined
Mar 26, 2020
Posts
8
Reaction score
3
Moshi.

Miundombinu kwenye masoko yaliyo mengi katika jimbo la Vunjo imetajwa kutokwa rafiki hivyo kufanya biashara kufanyika kwenye mazingira magumu na hatarishi ikilinganishwa na maeneo mengine nchini.

Kutokana na hali hiyo muingiliano wa wateja umekuwa ni mdogo hivyo wauzaji kuuza bidhaa zao hususan mazao na mifugo kwa bei isiyoendana na gharama za uzalishaji na kufanya kutopata faida.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye ofisi za CCM kata ya Kirua Vunjo Kusini mgombea ubunge jimbo la Vunjo (CCM)Dkt. Charles Kimei alisema mazingira yakuendeshea biashara ni lazima yakaboreshwe ili kuvutia wanunuzi wengi.

Alisema masoko yakiwa na miundombinu mizuri itaweza kuvutia wanunuzi wengi hivyo kukuza ushindani wa kibiashara na hatimaye kukuza kipato cha wakulima na wafugaji katika jimbo hilo.

Kwa mujibu wa Kimei ni kuwa masoko yakiboreshwa yataweza kuvutia watalii kufanya manunuzi katika eneo la Vunjo tofauti na ilivyo sasa kuwa wanaenda jijini Arusha na maeneo mengine hivyo kufanya mzunguko wa fedha kuwa chini.

''Ukiwa na masoko ambayo ni mazuri ni dhahiri kuwa kutakuwa na muingiliano wa watu wengi na hapo ndipo ubunifu wa kibiashara unapoanzia na kuanza kukua kwa kipato''alisema

Dkt. Kimei alisema baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwezi octoba ni lazima atumie elimu yake katika utaalamu wa fedha kuviwezesha vikundi vya vijana,walemavu,na akina mama namna yakuchangamkia fursa za mikopo.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imetilia mkazo kwa kila halmashauri kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mkopo usiokuwa na riba lakini ni watu wachache sana wenye uelewa katika hilo.

Samwel Shao ni mgombea udiwani kata ya Mwika Kaskazini (CCM)ambapo alisema baada ya kuchaguliwa ni lazima aanze na vikundi vya vijana na wanawake ili ahakikishe nao wanafaidi keki ya taifa kama ilivyo kwa maeneo mengine.

Alisema fursa za kujikwamua kiuchumi zipo ila tatizo ni kukosa uwakilishi sahihi wenye kuwa na maono na nia njema ya mafanikio badala yake ni uwepo wa wawakilishi wenye ubinafsi.

Mwisho.
 
Safi ila Kimei kama mkazi wa Vunjo alipaswa kuwa ameshaingilia na kushauri kuhusu hayo mambo mda mrefu ila yote kwa yote namtakia kila la kheri katika kuijenga mama Tanzania
 
Back
Top Bottom